Rais Magufuli kwa utendaji huu tutakupa vipindi kama vya Nyerere

Ni ukweli ulio wazi hata kwa wapinzani kuwa rais kafanya kazi kubwa kwa kipindi kifupi sana. Awali nilimuita Nyerere Junior na kwa kuwa Nyerere alitawala nchi hii kwa miaka 25, nashauri Rais Magufuli aongoze kwa muda kama huo ili nchi yetu isonge mbele kwa haraka ya treni ya umeme.

Kwa mwaka mmoja karudisha nidhamu kwa watumishi wa umma na watendaji wa serikali na mashirika ya umma, kwa mwaka mmoja kanunua ndege tatu na tayari mchakato wa ndege tatu zaidi umekamilika.

Kwa mwaka mmoja katimua watumishi hewa elfu kumi na tisa waliokula bila kutokwa jasho. Kwa mwaka mmoja kajenga barabara za rami zaidi ya kilometa 100 nchi nzima

Kwa mwaka mmoja GDP imepanda kwa 30%.

Kasi hii haijawahi kufanywa na rais yeyote tangu uhuru.Tuna imani naye na tutazidi kumchagua. Viongozi wa chama chetu anza utaratibu wa kubadili muda wa rais kukaa madarakani.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ignorance is bliss!!!!
 
FB_IMG_1481261721172.jpg
 
ZIPO CLIPS KIBAO HTA HAJAWA RAIS AKIZUNGUMZA GRAMMATICAL ENGLISH.BY THE WAY WHAT IS THE AIM OF LANGUAGE? RAIS WA CHINA ANAZUNGUMZA LUGHA GANI? NI MJINGA KAMA WEWE ANAYETUKUZA LUGHA ISIYO YAKE.ASILIMIA 70 YA WATAZANIA UKIWAMO WEWE HAWAJUI KIINGEREZA HALAFU YEYE ANG'ANG'ANIE KIMOMBO KWANI NI RAIS WA UINGEREZA?
Ni malkia was uingereza!!
 
Dah bado tunasafari ndefu kama taifa. Kwahiyo hiyo ndiyo inaitwa GDP? Kwahiyo TRA kila mwezi wanatangaza GDP ya nchi? So kila mwezi una GDP yake? Mbona tunaambiwa uchumi unakuwa kwa 7% kwa mwaka mbona ww hiyo GDP yako inakuwa kwa 30%?
Ndio maana tulisema Elimu, Elimu Elimu!!
 
watu kamaa nyie kila awamu mnakuwepo au kwa jina maarufu wapambe ambao kazi yenu kubwa ni kujipendekeza kwa viongozi walioko madarakani bahati nzuri rais wa awamu ya kwanza aliligundua ndio maana akaweka msisitizo kwenye katibaa ya nchi kuwe na ukomo wa kipindi cha kutawala hatuhitaji Magufuli kama mtu bali tunahitaji katiba bora ambaye kila kiongozi atakayeingia madarakani ataizingatia
 
Respect mkuu this is the best comment of the year. Tujenge mfumo mzuri kama nchi za wenzetu kiasi kwamba hta akija raisi mbovu bado nchi haiwezi kutetereka maana upo mfumo imara wa kuhakikisha mambo ya nchi yanaflow vzuri muda wote kuliko kuweka imani kwa mtu afu mwisho wa siku akistaafu tuanze tena MOJA. Congrats kwa kuliona hili
 
Ni ukweli ulio wazi hata kwa wapinzani kuwa rais kafanya kazi kubwa kwa kipindi kifupi sana. Awali nilimuita Nyerere Junior na kwa kuwa Nyerere alitawala nchi hii kwa miaka 25, nashauri Rais Magufuli aongoze kwa muda kama huo ili nchi yetu isonge mbele kwa haraka ya treni ya umeme.

Kwa mwaka mmoja karudisha nidhamu kwa watumishi wa umma na watendaji wa serikali na mashirika ya umma, kwa mwaka mmoja kanunua ndege tatu na tayari mchakato wa ndege tatu zaidi umekamilika.

Kwa mwaka mmoja katimua watumishi hewa elfu kumi na tisa waliokula bila kutokwa jasho. Kwa mwaka mmoja kajenga barabara za rami zaidi ya kilometa 100 nchi nzima

Kwa mwaka mmoja GDP imepanda kwa 30%.

Kasi hii haijawahi kufanywa na rais yeyote tangu uhuru.Tuna imani naye na tutazidi kumchagua. Viongozi wa chama chetu anza utaratibu wa kubadili muda wa rais kukaa madarakani.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Hii ndio shida ya kukurupuka.. SIZONJE kawapatieni ugonjwa mubayya sana
 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kigumu chama cha Mapinduzi! Mkereketwa mwenzangu, Nyerere kadumu muda m,refu sio kwa sababa ya kupendwa au kwa uongozi bora ulioutukuka lakini ni kwa fimbo ya chuma. Kulikuwa hakuna uchaguzi wa demokrasia.

Nchi ilisambaratika,watu wakawa masikini wakutupwa hata kukkosa sabuni ya kuoga na kufulia,, Njaa iliokithiri mpaka ikiwalizimu watu waishi wa chakula cha msaada wa sembe lamanjano (sembe la Yanga).Tanzania ikawa Imefilisika. Kuona nchi kaifikisha mrama ndipo alipo achia ngazi tena mguu mmoja mwengine akautumia kuharibu ya mrithi wake.
Sasa wewe unataka tuelekee huko? God forbids.Mwache JPM jenge himata yake atawale hata maisha lakini isiwe kwa legacy ya Nyerere
 
Acheni kujitoa akili nyie maccm!!! Huyu mtu ana degree tatu je huko chuoni walikua wanatumia kiswahilli??? Kwa lugha anayoongea huoni alikua anachungulia darasan??
Ndo maana nasema ukobonzi Wa fikra na elimu inaitajika sana kwako, you can be good in writing but no fluent, na ubora Wa kuongea hauna uhusiano wowote na kua kiongozi mzuri,
 
Ndo maana nasema ukobonzi Wa fikra na elimu inaitajika sana kwako,
Nadhani ukombozi wa fikra unahitajika kwako zaidi na huyo mnayemtetea humu, maana wote ni kama mna akili zinazofanana!
you can be good in writing but no fluent,
Unaelewa maana ya fluent wewe gamba??? unasemaje una phd wakati kuunga sentensi kwa lugha uliyoitumia kupata hiyo degree unashindwa??
na ubora Wa kuongea hauna uhusiano wowote na kua kiongozi mzuri,
Mkuu unajua maana ya kiongozi? unaelewa maana ya kiongozi mzuri?? je huyu unayemtetea hapa ni kiongozi?? na ni nani kaongelea maswala kiongozi hapa??
 
Back
Top Bottom