Tanzania imejengwa katika misingi ya amani japo, amani hii wakati mwingine haina tofauti sana na maigizo ya kaole lakini waliokutangulia waliweza kuigiza vizuri wakamaliza muda wao.
Ni kweli hata huko nyuma watu walikua wakiuawa kinyama wengine kwa kuchinjwa, wengine kwa kuchomwa moto na wengine kwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha lakini mtanzania alipomtazama kiongozi wake waliona amani maana hata kiongozi akisisimama jukwaani alionekana kukerwa na kuwa kinyume na yanayotokea kwa hiyo mtanzania alipongeza kwa kuwa ndani ya nchi ya amani kwakua.
Swala la kuzuia haki ya vyama vya upinzani kuzungumza na wananchi wao huku kina Mwigulu wakipeta na mikutano ya hadhara kila wanapotaka, tena bila bugudha yoyote na wewe Mh. Rais umekaa kimya! Ni hatari sana, watanzania wa sasa sio wale wa mwaka 61 hawa japo hujashtuka wanaelewa. Kwa hiyo kwa kuamua kukaa kimya huku wapinzani wakinyimwa haki yao ya msingi unawafanya watanzania wathibishe kile wanachokihisi kuwa wewe ni dikteta.
Mh mama mmoja aligombana ama alipishana kauli na afisa usalama barabarani na mara moja ulijitokeza ukuongea kwenye vyombo vya habari na ukampandisha cheo yule askari japo mkuu wake alisema zipo taratibu kwahiyo hakufanikiwa, lakini unashindwa kusimama ukawaambia Polisi waache dhuluma wanayowafanyia wananchi kuwanyima hali ya kuwasilikiza watu wao waliowachagua kwa halali kabisa! Mh hili ni jipu na usipoangalia linatumbuka 2020.
Ulipozungumza na wazee wa Dar es Salaam ulisema swala la lanzbar hutojihusisha nalo unakaa kimya ila ukaseman walete fyofyoko waone! sasa hii kauli hadi leo watanzania nikiwemo mimi wanajiuliza hii kauli maana yake ninini? maana yake nini......
Mh Watanzania wana maumivu mengi sana lakini wanaogopa kusema ukweli sasa, usiposhtuka 2020 hawataangalia push-ups maana na zenyewe wameanza kuona kwamba labda hazikua na maana nzuri kwao..Utawala bora Mh lazima uruhusu watu kuwasiliana bila kujali itikadi ya vyama vyao
Haya mambo usiyachukulie hasira Mh, Mungu aliyekuumba na pua inayoangalia chini akusaidie uelewe kwamba nchi lazima iongozwe kwa misingi ya demokrasia vinginevyo 2020 utakumbuka huu uzi utakapomuona Lowasa aliyeitwa mfu anayetembea akiingia Magogoni bila kutumia jasho.