Rais Magufuli kuzindua jengo la Mfuko wa PSPF na tawi la Benki ya NMB Jumatatu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Dodoma. Rais John Magufuli kesho kutwa (Jumatatu) atazindua jengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF na tawi jipya la Benki ya NMB lililopo Mtaa wa Barabara ya Chimwaga mjini Dodoma.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema Rais Magufuli atawasili kesho mjini hapa.

“Siku ya Jumanne Aprili 23, Rais atakuwa mgeni rasmi kulihutubia Bunge la Afrika Mashariki ambalo linafanyika Tanzania Bara hapa Dodoma,”amesema.

Amesema Alhamisi Rais atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika katika uwanja wa Jamhuri.

“Siku ya Ijumaa Rais atazindua barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa Kilometa 231.8 na sherehe ya uzinduzi wa barabara hii zitafanyika kwenye wilaya ya Kondoa eneo la Bicha,”amesema.

Amesema uzinduzi wa barabara hiyo ni kichocheo kikubwa cha shughuli za uzalishaji na uchumi wa ukanda wote wa Bahi, Chamwino, Chemba na Kondoa.

“Nisisitize kuwa barabara hii ni sehemu ya Barabara kuu ya kaskazini (Great North Road) inayoanzia Cape Town Afrika Kusini hadi Cairo Misri hivyo ina umuhimu wa kipekee kwetu wananchi wa Dodoma upande wa shughuli za uzalishaji viwanda na uchumi,”amesema.

Dk Mahenge amesema Jumapili Rais ataondoka kulekea mkoani Iringa kwa ajili ya Sherehe za Mei Mosi kitaifa mwaka huu ambazo zinafanyika kitaifa mkoani humo.

“Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma namshukuru Rais Magufuli kwa heshima hii ya kipekee anayoendelea kutupatia sisi Mkoa wa Dodoma ambayo ni Makao makuu ya nchi,”amesema.

Amewataka wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano
Source: MCL
 
Ila kwa sasa rais wetu anatia aibu, kitawi cha benki tu nacho anazindua yeye? Au ndio kule kukosa kazi za kufanya!
 
Tunataka pesa zetu, na sio majibu mepesi mepesi na kutufanya sisi watanzani wajinga au hatuja elimika.
tapatalk_1523941642385.jpeg
 
Kwa mara ya nane nasubiri kusikia "tumeongeza bajeti ya afya kutoka 32 hadi 260 bilioni" nadhani hakuna kete iloyobakia.
 
Siku hizi raha sana , ratiba za rais zipo hewani kama ratiba za show za diamond.

Mkuu mtake radhi diamond,shows zake ni adimu sana!!!! Ataenda hapo kuzindua kajengo kaghorofa 2 na msululu wa mawaziri. Serikali ya kubana matumizi!!!

Nyumbani kwangu vibaka walikuwa wanaiba sufuria na nguo kwenye kamba sasa nimezungushia ukuta-naombeni msaada kwa wahusika waje wauzindue!!
 
kiukweli 1.5 imempunguza makali,hata makeke yamemuisha
ufisadi hauna mwenyewe as long as upo ccm utafisidi tu at some point
 
Mkuu mtake radhi diamond,shows zake ni adimu sana!!!! Ataenda hapo kuzindua kajengo kaghorofa 2 na msululu wa mawaziri. Serikali ya kubana matumizi!!!

Nyumbani kwangu vibaka walikuwa wanaiba sufuria na nguo kwenye kamba sasa nimezungushia ukuta-naombeni msaada kwa wahusika waje wauzindue!!
Andaa utepe na mkasi. Tunakuja kuzindua.
 
Namuomba aje na huku mkoani afungue kilabu cha mbege hapa kirema sokoni moshi kuna kiwanda cha kutiisha mbege
 
Back
Top Bottom