Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi ujenzi wa FLYOVER TAZARA, kufungua daraja la Kigamboni Aprili 16

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
549
613
Waswahili husema '' Hayawi hayawi sasa yamekuwa".Hatimaye ule uzinduzi wa daraja la kigamboni na ufunguzi wa ujenzi wa flyover ya Tazara uliokua ukisububiriwa na wananchi wengi wa Dar es Salaam kufanyika ndani ya siku moja yaani Jumamosi ya tarehe 16 mwezi huu.

======

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA NA KUFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI JIJINI DARA ES SALAAM

taza.jpg

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).

Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi huu umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Aidha wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.

Utekelezaji wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga

Katibu Mkuu (Ujenzi)

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

14 Aprili, 2016
 
China wamefungua daraja lenye urefu wa km 41.3 baharini na limegharimu USD 1.4B...

Daraja letu la Kigamboni lina urefu wa mita 600 baharini na limegharimu USD million 136 - 218.

China: 1,400,000,000÷ 41300=

33,898.305085 USD, kwa Ujenzi wa mita moja ya Daraja China.

Tz: 218,000,000÷600=

363,333.33 USD kwa ujenzi wa mita moja ya daraja la Kigamboni Tanzania

Muda wa ujenzi kwa madaraja yote ni miaka minne kila moja, Analysis ya muda uliotumika kwa km 41.3 ni sawa na mita 600

NSSF huenda ipo sayari nyingine sio hii iitwayo dunia.

Maajabu yataisha lini Tanzania?
 
China wamefungua daraja lenye urefu wa km 41.3 baharini na limegharimu USD 1.4B...

Daraja letu la Kigamboni lina urefu wa mita 600 baharini na limegharimu USD million 136 - 218.

China: 1,400,000,000÷ 41300=

33,898.305085 USD, kwa Ujenzi wa mita moja ya Daraja China.

Tz: 218,000,000÷600=

363,333.33 usd kwa ujenzi wa mita moja ya daraja la Kigamboni Tanzania

mkuu uko sirias??! daraja lina km 41?? em tupe source
 
Daraja la km 41?
 
Mi Naonaga Kulalamika Kwa watanzania Kupo Damuni

Lisingejengwa ungesema Mengine
Limejengwa ushaleta mahesabu ya darasa la Saba...

Kama ufisadi Upo si magufuli atatumbua....
 
China wamefungua daraja lenye urefu wa km 41.3 baharini na limegharimu USD 1.4B...

Daraja letu la Kigamboni lina urefu wa mita 600 baharini na limegharimu USD million 136 - 218.

China: 1,400,000,000÷ 41300=

33,898.305085 USD, kwa Ujenzi wa mita moja ya Daraja China.

Tz: 218,000,000÷600=

363,333.33 usd kwa ujenzi wa mita moja ya daraja la Kigamboni Tanzania

Muda wa ujenzi kwa madaraja yote ni miaka minne kila moja, Analysis ya muda uliotumika kwa km 41.3 ni sawa na mita 600

NSSF huenda ipo sayari nyingine sio hii iitwayo dunia.

Maajabu yataisha lini Tanzania?
Hata ungeenda wapi cost zisingeweza kufanana sababu kuna utofauti wa gharama za factors of production kati ya tz na china kumbuka hilo.
 
Back
Top Bottom