Rais Magufuli Kuwa Kama Donald Trump Kuhusu hizi Fake News

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Toka kampeni zake za urais na mpaka baada ya kuwa Rais Donald amekuwa akiandamwa na vyombo vya habari haswa Main Stream News, imefikia hatua utawala wa Donald Trump kuzipiga marufuku mashirika za habari kama CNN kuripoti habari kutoka ikulu.
Kama ulivyozungumza jana vyombo vya habari hapa nchini zimeanza kujitokeza tabia ya kupiga vita viongozi wa serikali yako, mheshimiwa rais wewe chapa kazi wala usisononoke hivi vyombo miongoni mwao vitakufaa natural death. Wewe ndio kiongozi pekee baada ya Edward Sokoine kuwahi kutokea hapa Tanzania kuonyesha dhamira wazi watanzania kuwa unaweza kufanya maamuzi bila kufumba macho wala kubabaika.
Ili kurudisha heshima ya nchi hii na kufuta ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na vita dhidi ya madawa ya kulevya kiongozi shupavu kama wewe unahitajika.
Kuhusu wewe kumtetea Makonda una haki kubwa ya kumlinda huyu kijana kwani amekuwa msaada mkubwa sana kwako hasa katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Kuna dalili za fedha za hawa mafisadi na wauza madawa za kulevya zimeanza kutumika kwenye vyombo vya habari katika kuchafua serikali yako, mheshimiwa Rais Magufuli inabidi na wewe ufate mkondo wa Donald Trump wa kuzipiga maarufuku vyombo hivyo katika shughuli zozote za serikali. Na hata haya matusi katika mitandao ya kijamii dhidi yako ni hao hao mafisadi na wauza madawa na baadhi ya vijana wasiojua maana ya kutumia mitandao ndio wanatumika lakini siku zote watashindwa kwa uongozi wako wa kijasiri uliouonyesha.
Mheshimiwa Rais wewe chapa kazi wala usikatee kwani utaingia katika historia ya nchi hii kama kiongozi shupavu.
 
CNN imepigwa marufuku ikulu ya Marekani?

Hebu acha kusambaza fake news na wewe!
 
Awe kama Trump, yaani afute misaada kwa nchi za hovyo, azuie raia wa nchi baadhi kuja Tz, na siku akiwa na press TBC inayopendwa pamoja na Uhuru gazeti ndio wakaripoti kutoka Ikulu.
Hujastuka juzi kilichotokea bandarini? TBC, Uhuru, Habari Leo walikuwepo ila nafikir umeona kikichotokea.
 
Back
Top Bottom