Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Ni wazi kwamba CCM wako njia panda. Wanajiuliza nini zitakazokuwa athari za utawala wa Raisi JPM kulekea uchaguzi wa 2020. Je, staili yake ya uongozi itaporomosha umaarufu wa CCM kwa wapiga kura? Italeta mgawanyiko ndani ya CCM? Wanajiuliza pia, kama kuna uwezekano wa hayo kutokea, isingekuwa vema asiwe Mwenyekiti wa CCM ili angalau kuwe na Mwenyekiti wa CCM tofauti ili kudhibiti mambo na hali ikiwa mbaya wavunje rekodi yao na kutomteua kuwa mgombea wa Uraisi wa CCM itakapofika uchaguzi wa 2020? Ni wazi kwamba Raisi Magufuli akijua hili, atataka sana awe Raisi na Mwenyekiti wa CCM, ili kujihakikishia kuteuliwa tena kuwa mgombea wa CCM 2020.
Na pia, ni wazi kwamba, kama CCM wataona kwamba staili ya uongozi wa Raisi Magufuli inaathiri kukubalika kwa CCM kwa wapiga kura, basi watafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba wanadhoofisha upinzani nchini, ili kwamba hata kama umaarufu wa CCM utapungua, basi kusiwe na chama cha siasa cha upinzani chenye nguvu na kutumia nafasi hiyo na kuiondoa CCM madarakani hapo 2020.
Haya, sisi wengine ni watazamaji tusiofungamana na upande wowote. Ngoja tuone itakavyokuwa.