Rais Magufuli kutokusafiri nchi za nje, anastahili pongezi na mtu aliyeiona kesho

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Kwakweli ukiangali mikutano na warsha mbalimbali viongozi wetu wanazokwenda kuhudhuria nchi za nje ni upuuzi mtupu

Kwa mfano huu mkutano wa juzi Urusi na ule wa China wa kuwaalika viongozi wetu hauna afya kwa bara letu zaidi ya ukoloni mamboleo.

Africa itajengwa na waafrika wenyewe kupitia viongozi wenye maono kama Rais Magufuli na Paul Kagame.

AU na wadau mbalimbali kupitia secretarieti zao wanatakiwa kuwa na jopo la watu wenye vision ambao watasaidia bara hili kujikwamua na sio kuomba misaada tu.

Africa inaweza kujisimamia kwa maana sie tuna rasilimali na malighafi za kutosha zaidi na pia tuna soko kubwa la kuuziana wenyewe.

Rai yangu kwa viongozi wa Africa ni kwamba tunatakiwa kujimwabafai na rasilimali zetu ili ziweze kuwaletea wananchi wetu maendeleo.

Rais wetu Magufuli ana jicho la tai kukwepa mialiko ya nje ambao kimsingi ni gharama kwetu na zaidi haina tija zaidi ya kuja kuwa mauti kwetu.

Alex Fredrick

Morogoro.
 
Africa inaweza kujisimamia kwa maana sie tuna rasilimali na malighafi za kutosha zaidi na pia tuna soko kubwa la kuuziana wenyewe

Rai yangu kwa Viongozi wa Africa ni kwamba tunatakiwa kujimwabafai na rasilimali zetu ili ziweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo

Rais wetu Magufuli ana jicho la Tai kukwepa mialiko ya Nje ambao kimsingi ni gharama kwetu na zaidi haina tija zaidi ya kuja kuwa mauti kwetu

Alex Fredrick

Morogoro
Naona mkata viuno umesogea mbele unaserebuka kweli kweli!!
 
Rais wenu ni mgonjwa sio hataki kusafirii nje. Betri likichomoka huko Angani itakuwa taabu.
 
Africa inaweza kujisimamia kwa maana sie tuna rasilimali na malighafi za kutosha zaidi na pia tuna soko kubwa la kuuziana wenyewe.

Rais wetu Magufuli ana jicho la tai kukwepa mialiko ya nje ambao kimsingi ni gharama kwetu na zaidi haina tija zaidi ya kuja kuwa mauti kwetu.
Alex Fredrick
Morogoro.
Mkuu Alex Fredrick, kwanza naunga mkono hoja rais Magufuli kutosafiri nje safari za hovyo hovyo, na pia Afrika tuna rasilimali nyingi za kutosha kutuletea maendeleo, tatizo ni mitaji ya kuvuna rasilimali hizo na teknolojia ya kuzibadili kutuletea maendeleo, hatuna na inatubidi kuendelea kuwategemea mabeberu!. Hivyo ziko safari muhimu za heads of state and governments, ambazo zinahusu mustakabali wa nchi kwenye regional integration na some international conferences, rais wetu Magufuli lazima eande in person ili kujiunga na wenzake na kujichanganya na sio kila uchwao yeye ni kuwakilishwa tuu. Atapata wapi international exposure?, mwisho atakuja kujikuta yuko out dated and out of place!.
P
 
NYIE HAMMJUI MAGUFULI AWAMU HII YA PILI, ATAONGOZA TANZANIA AKIWA ANAISHI QATAR. MWANA SIASA HUYO OOOHOOO! ANAKUSANYA KWANZA HELA!

ATASEMA HIVI, ''MUNGU AKIKUPA NCHI NI AMEKUPA!
 
Hahaha kiswahili SADC anafundisha online?! Alipaswa kuwatembelea wanafunzi wake japo mara moja kwa mwaka.
 
Huyu rais ametengeneza rekodi mpya na kudhihirisha kwamba inawezekana kwa nchi ya Kiafrika kupiga hatua kimaendeleo bila rais wake kuzurura kwenye mataifa ya watu.
 
Hivi mnajua umuhimu wa international diplomacy au mnaongea ujinga, kwamba kila analoamua Mh. Nikushangilia tu? Hao wazungu wametuzidi mambo mengi an, hata Rais wa China anaenda huko sembuse sisi omba omba hadi wa neti? Ebu tuache kiburi kisichotusaidia chochote, we need them more than they need us! Only a fool will argue otherwise!!
 
Huyu rais ametengeneza rekodi mpya na kudhihirisha kwamba inawezekana kwa nchi ya Kiafrika kupiga hatua kimaendeleo bila rais wake kuzurura kwenye mataifa ya watu.
Ndio maana kuna uhusiano wa kimataifa, rekodi inayotengenezwa ni ya ajabu, haipo, hata huyo kagame anaenda huko, hamna maendeleo duniani bila kushirikiana na mataifa mengine! Umeendelea kwa lipi hadi ujitenge?
 
Yani nyie ndio mnazidi kumpotosha mkuu nafikiri ujui umuhimu wa baadhi ya ziara za wakuu wa nchi wazifanyazo, marekani na China pamoja na uchumi wao imara marais wao wanatoka sembuse sisi ngulumbili, eti afrika tuna rasilimali sawa ni kweli lakini bila teknolojia akuna maendeleo.

Kumbuka kuwa teknolojia yote ipo kwao hao mnaowaita mabeberu,pia viongozi wetu afrika si wazalendo ni wabinafsi walafi na ving'ang'anizi wa madaraka ndugu yangu bila kutumia akili na kushirikiana na hao mabeberu maendeleo ni ndoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kushirkiana haimaniishi uhudhurie kila kikao kukenua meno huko, rais Magufuli anakatiza nchi yote, mara yuko Lindi, mara Tunduma yaani hadi raha, anakwenda kote na kutatua kero za wananchi. Maana viongozi kule mikoani walikua wamezoea kuishi kwa mazoea, sasa rais huyu anawakuta huko huko na kuhakikisha wanawajibika.
 
Hiy
Yani nyie ndio mnazidi kumpotosha mkuu nafikiri ujui umuhimu wa baadhi ya ziara za wakuu wa nchi wazifanyazo, marekani na China pamoja na uchumi wao imara marais wao wanatoka sembuse sisi ngulumbili, eti afrika tuna rasilimali sawa ni kweli lakini bila teknolojia akuna maendeleo.

Kumbuka kuwa teknolojia yote ipo kwao hao mnaowaita mabeberu,pia viongozi wetu afrika si wazalendo ni wabinafsi walafi na ving'ang'anizi wa madaraka ndugu yangu bila kutumia akili na kushirikiana na hao mabeberu maendeleo ni ndoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo technology ndiyo inamfanya asisafiri safiri na akaweza kumudu international diplomacy bila wasi wasi. Maana uina vitu kama video conferencing n.k, ambavyo anaweza akaongea na walengwa bila yeye kuwepo physically! Na akawa ameserve hela nyingi.. Yeyote anayefikilia Rais ange safiri nje kila mara anajifikiria mwenyewe ili apige hela {yaani kama angekuwa Rais)!
 
Back
Top Bottom