Benz Petrol
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 504
- 196
Habari wanajamvi,
Tokea achukuwe madaraka, Rais Dkt J.P. Magufuli amaonyesha nia na dhamira kwa vitendo na kwamba serikalini hakutakuwa na 'business as usual'. Rais amtokea kuwa mtu asiyetabirika katika maamuzi yake na kuonyesha kuchikizwa wazi wazi na wazembe, wala rushwa, mafisadi n.k.
Rais katika 'utumbuaji' wake amewakumbusha watumishi wote wa umma kwamba uadilifu ni jambo muhimu mahali pa kazi, pia kadhihirisha haangalii muda gani amemteua kiongozi au muda gani ametumikia nafasi aliyopewa (mfano Kilango, Kitwanga), bali kinachoangaliwa ni utendaji kazi wake kwa taifa na kwa waTanzania kwa ujunla.
Rais ameoneshwa kuwa haendeshwi kwa siasa za vyama kwa kuangalia wanasiasa (wa chama tawala au upinzani) watasema nini na pia amekua akisema hii ni 'serikali ya Magufuli'. Kwa mantiki hiyo kuna kila uwezekano wa Rais kuteua Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nje ya mfumo wa CCM na hata kutoka upinzani. Mh. Rais anahitaji mtu wa kuendana na spidi yake na kwa maoni yangu mtu huyu kwa sasa hayupo ccm. Karibuni tujadili.