Rais Magufuli kutembelea Arusha kwa njia ya barabara akitokea Dodoma

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Rais Magufuli leo atasafiri kutoka Dodoma kuelekea Arusha kupitia Mkoa wa Manyara kwa njia ya Barabara.

Rais atatumia nafasi kukagua ujenzi wa barabara ya Babati mpaka Dodoma kupitia Barabara kuu ya Kondoa ambayo ni kiunganishi cha mikoa ya Kaskazini na Kusini.

Rais pia atatumia muda kuangalia athari za mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika vijiji vilivyoko pembeni mwa barabara ya Dodoma-Arusha.

Kuna uwezekano wananchi wa maeneo ya Kondoa, Babati, Monduli, Manyara na Arusha watapata fursa ya kuongea naye ana kwa ana kwa sababu ni kawaida yake kuwasikiliza wananchi moja kwa moja kwa kutumia dhana ya HapaKaziTu.

Akiwa Arusha, Rais atahudhuria sherehe za Kijeshi kwa waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika chuo cha Kijeshi ambacho kipo wilayani Monduli.

Baadae atafungua Jengo la Mfuko wa PPF katika eneo la Uzunguni Arusha.
 
Baadaye atafungua Jengo la Mfuko wa PPF katika eneo la Uzunguni. Arusha.

Meambieni nchi hii sio ma barabara tu. Kuna mambo mengi ya nawasimbua watanzania
 
huyu ndiye raisi aliyekuwa anasubiriwa na wanyonge wa nchi hii
kila mwananchi wa chini ana matumaini makubwa na raisi.
karibu jpm arusha tuko pamoja,

wale wengine wamebaki kuwa watetezi wa mafisadi nadhani mda si mrefu watapotea.
 
4d26f11e26882dff9e1775d34738722f.png
 
Meambieni nchi hii sio ma barabara tu. Kuna mambo mengi ya nawasimbua watanzania
Kabla ya kuanza kubeba kazi ya kutoa ushauri kwa Rais wa Tanzania, nenda kwanza ukajifunze kuandika na kusoma kwa ufasaha.

Wewe hata basic knowledge huna, utaiweza kazi ya kutoa ushauri kwa Rais wa Tanzania?

Hii nchi ina vituko!
 
Back
Top Bottom