Wakati wa utawala wa mkapa alijiwekea utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara moja kwa mwezi kwa lengo la kubadilishana mawazo na kushauriana. Napendekeza na kwa utawala huu kiongozi wetu aweke utaratibu wa kukutana na wawakilishi wa chama cha wenye viwanda (CTI), chama cha wafanyabiashara TCCIA na baraza la taifa la biashara TBNC angalau mara moja kwa mwezi na badae anaweza punguza kulingana na maendeleo ya majadiliano.
Navyoona huyu waziri mwijage sidhani kama anakotupeleka ndiko tunakotakiwa kwenda, ukweli anahitaji maarifa zaidi ya hayo aliyonayo, niseme machache.
Ukweli ni kuwa vyanzo vya ajira vinazidi kupungua na wasaka ajira wakizidi kuongezeka, na tuseme ukweli wanaohangaika na ajira sehemu kubwa ni vijana. Hili la kusema vijana wajiajiri kwenye ujasiliamali naona tunawaonea tu, waliopaswa waambiwe ni wazee walio na mitaji kutokana na mafao yao ya utumishi, walio na weledi kutokana na kufanyakazi muda mrefu na kuwa na weledi na uzoefu wa kutosha, sasa kama hawako tayari hawa vijana tunawaonea tu bure.
Ukweli huwezi anzisha kiwanda ukafanikiwa bila kulindwa na serikali, bila kuwepo sera madhubuti na mipango inayotekelezeka. Hatuwezi sema tuwe na viwanda hivi hivi pasipo kuwa na sera ya kulinda hivyo viwanda, viwanda vinahitaji mtaji mkubwa na urejeshwaji wake ni wa taratibu na muda mrefu, hivyo mwekezaji anahitaji kuhakikishiwa sustainability katika biashara yake.
ukweli viwanda Tanzania haviendesheki kwani mazingira ya kisera sio rafiki, na watunga sera hawajui nini hasa kinahitajika kwanza wao wenyewe hawana ujuzi na kama wanao basi ni ujuzi mbovu na wengi wao wametoka katika viwanda au mashirika yaliyoshindwa ku perform.
Mfano, kwa utawala wa mwalimu alijenga viwanda vinne vya sukari ndani ya miaka 25, leo miaka 30 tangu mwalimu aondoke hata hivyo vinne alivyoacha mwalimu tumeshindwa kuviendesha na kuzalisha sukari ya kutosha kulisha watu wetu achilia kuuza nje ya nchi.
JK aliweka mazingira mazuri ya kuendesha vyuo vikuu, ndani ya miaka kumi tayari tunavyo vyuo vikuu 45 na vinadahili wanafunzi zaidi ya elfu 120 kutoka wanafunzi elfu tatu wa awali, tukigeuza mkasi kidogo tu ndani ya mika kumi tutabaki na vyuo vikuu vitatu na ndiko tunako elekea. Ndivyo hivyo hivyo na viwanda na mashirika ya kibiashara, tukiweka sera sahihi basi tutafikiwa lengo kusudiwa.
Lakini hatuwezi kufika huko kama tutategemea watu walioshindwa kuendesha stamico nbc nhc tirdo narco nafco halafu haohao eti leo watufikishe kwenye uchumi wa viwanda, hapana tunadanganyana.
Tuwaite akina Mengi Bhakresa Somaia Gachuma Shirima Karimjee Rajan Cotak tuwaulize tunawezaje kukuza sekta ya viwanda na kuongeza ajira? Angalia mashirika ya usimamizi yako busy kukimbizana na wafanyabishara, nemc funga kiwanda, tfda choma vipodozi, sumatra kamata mabasi, eura funga vituo vya mafuta, tcra zima simu, lakini hakuna hata mmoja kati ya hawa aneakaa chini na wafanyabiashara na kushariana nao njia bora ya ufanyaji biashara pasipo kuathiri mazingira na pasipo kukiuka sheria.
Tunachoma vipodozi kila siku mbona hatumkamati aliyeruhusu hivyo vipodozi kuingia? tunachoma nyavu wakati nyavu hizo hizo zinauzwa madukani na hatuzikamati kwanini? Tunazima simu feki wakati simu hizo zimeagizwa kihalali na zimelipiwa kodi na madukani zipo zinauzwa huko si ni kukatana mtaji? Kama tumebadili sera na hatutaki simu feki basi kwanini tusiwalipe fidia waliongiza hizo simu na kulipa kodi halali?
Hivi tulishajiuliza kabla ya kufungua kiwanda mtu anahitaji vibali vingapi? na vinachukua muda gani? na kunachangamoto kiasi gani? na mtu akileta contena la mitumba anapitia hatua ngapi linakuwa sokoni tayari?