VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mara kwa mara umekuwa ukilaamu kuhusu Serikali kupitia kwa DPP na AG kushindwa kesi mahakamani. Hata jana, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini, umeligusia hilo na kuonesha kukerwa nalo. Unatamani Serikali ishinde kila kesi yake mahakamani!
Hilo haliwezekani. Haliwezekani kikatiba,kisheria na hata kimahakama. Nimekuwa Wakili kwa miaka 20 (kwasasa nimepumzika na nipo kisiasa zaidi) na siamini kuwa ni lazima kushinda kila kesi mahakamani. Mahakama ndiyo inayotoa uamuzi baada ya pande husika kusikilizwa.
Kazi ya Mawakili, ima wa Serikali au binafsi, ni kuishawishi Mahakama kuamua kwa upande wake. Mahakama hushawishiwa kwa kutafrisiwa sheria na kesi zilizokwishaamuliwa na mahakama katika jambo kama hilo. Mawakili si waamuzi, Mahakama ndiyo kila kitu. Ndiyo maana asiyeridhika hukata rufaa.
Kusemasema kwa kukereka juu ya kushindwa kesi kwa Serikali ni kuiweka Mahakama katika wakati mgumu. Ni kuishurutisha Mahakama 'indirectly'. Pia, hakutakuwa na mantiki wala maana ya kuwa na Mawakili wa kujenga hoja kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Hakutakuwa na haja kwakuwa mshindi 'atalazimishwa' kushinda.
Ingawa Mawakili jana walicheka uliposema vile, walipaswa kupenyeza maelezo kama haya ili ujue kuwa Mawakili wana mwisho wake katika kesi. Kinachotakiwa kwa Mawakili wa Serikali na wengineo ni kujiandaa na kupambana ipasavyo. Kushinda na kushindwa kuwe matokeo tu. Serikali nayo hushinda kesi za kutosha Mahakamani!
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam