Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,407
- 31,387
Najiuliza kama tusingekuwa na vyombo vya mawasiliano tungesikia nini!Umati mkubwa wa wananchi umelipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuaishwa kwa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa leo Jumamosi Mei 25, 2019
Hii ni exaggerations kubwa sana. Wafalme na viongozi wote walipata shangwe akiwemo De Klerk ambaye kulikuwa na sauti za zomea kidogo. Kwa ujumla Marais wote walishangiliwa
Ukiliacha jambo likatokea kwa njia za asili linakuwa bora zaidi kuliko jambo la kubumba
Ni jambo jema Rais wetu amehudhuria sherehe hizo.
Lakini pia kuna wakati maneno na exaggerations zinaweza kuwarudi wanaozieneza
Tuliambiwa kutosafiri ni kupunguza gharama. Sina uhakika kutumia dege la ATC kumesaidia gharama hasa ukilinganisha na ndege ya abiria kwa first au Business class kwa watu wachache kwani Ubalozi wetu na SA ungeratibu ziara nzima
Kesho kuna mtu atatupa excuse za gharama kwa mfano kutohudhuria SADC n.k.?
Wachumi watusaidie maana wengine namba zinatuchanganya, hasa 6 na 9 au 7 na L
JokaKuu Pascal Mayalla Mag3 tindo