Kitendo cha Rais Magufuli kumwita mwanamziki Ikulu ili kuongea naye ni UKOMAVU wa KISIASA.
Ninavyoona mimi polepole Magufuli anaanza kujua kucheza ligi ya siasa.
Siasa haihitaji kutumia NGUVU naAMRI kila wakati bali wakati mwingine ni UJANJA wa kisiasa.
Ujanja huo Mwalimu Nyerere aliujua sana. Tunaambiwa wakati wa Nyerere, kuna jamaa alikuwa ANAMPINGA sana. Siku moja askari walitumwa kwake kumchukuwa kwenda Ikulu. Jamaa huyo akajua sasa mwisho wake umefika.
Inasemekana alipofika huko Mwalimu alimkaribisha kwa tabasamu na chai mezani. Akamuuliza nasikia UNANISEMA sana niambie wapi NIMEKOSEA?.
Huyu jamaa bila woga alimwambia Mwalimu mahali palipokuwa panahitaji marekebisho. UGOMVI ukaishia hapo na huyo jamaa ALIBADILIKA na kuanza kutoa SIFA kemkemu jinsi mwalimu ni mtu MSIKILIZAJI mzuri na rais mzuri. Kisa? ALIPEWA SIKIO!
Katika hili rais Magufuli amefanya jambo la BUSARA sana. Maana si kila AKULAUMIAYE ni ADUI na huyo huyo anaweza kuwa msaada mkubwa sana POSITIVELY ukimhandle kwa hekima. Kwa hilo Magufuli nakupa hongera.!