Rais Magufuli, kumteua mtu na kumpa hisia hasi hapohapo tena za kumdhalilisha utu kabla hajaanza hata kazi si sawa

Mkuu umesoma science nini Tanzania

Umeshindwa kumuelewa Rais

Soma Fasihi,Rais aliongea vitu tofauti na fikra zako

Umechemsha mkuu,Ulisikiliza hotuba au umesimuliwa
Ungemuelimisha yeye na wengine kwa kuwapa fasihi sahihi ya yale aliyozungumza Mheshimiwa Rais.

Amandla....
 
Unaonesha ni mtu mwenye ufahamu finyu sana katika suala la kuchambua lugha zinazozungumzwaa na mtu kwa wakati na mahali alipo na jinsi ya kuhusianisha mazingira.. pole sana kiongozi

Mchambuzi feki wewe, hili halikuwa ni swala la lugha. Yalikuwa ni maneno ya kuonya tabia ya kugombea wanaume. Spin doctors mtakuja hapa na kujifanya mlielewa tofauti na msemaji - maneno huchukuliwa yalivosema na ndio maana ni muhimu mtu kusema mambo kwa tahadhari kwa sababu yakishasemwa yanabaki hivo hivo.

Mkuu, acha ujuaji njaa. Uchambuzi wa kidwanzi hautakiwi hapa. Point ni kuwa maneno hayo yalisemwa na acha watu wayazubgumzie kama yakivosemwa. Jambo lililozungumzwa kwa Mtela ni hilo hilo kwa DC na mwenzake amefukuzwa kazi.

Halafu unaleta udwanzi eti kuna swala la wakati na mazingira. Hivi upumbavu wa namna hii mtautoa lini vichwani??
 
Huwezi kuleta utani ambao ni matusi mbele ya hadhira. Kwa maana halisi, mwanamke anayegombea wanaume ni KAHABA au MALAYA. Jee Jokate anagombea wanaume?
Jee Jokate ni Malaya au Kahaba kulingana na maneno ya Rais?
Tabia hii ya kudhalilisha watu imeshika kasi na utetezi wenu ni kuwa anatania. Jee na yeye tumtanie atakaa kimya?
Tukimtania yy ni utakatishaji na uhujumu
 
Huwezi kuleta utani ambao ni matusi mbele ya hadhira. Kwa maana halisi, mwanamke anayegombea wanaume ni KAHABA au MALAYA. Jee Jokate anagombea wanaume?
Jee Jokate ni Malaya au Kahaba kulingana na maneno ya Rais?
Tabia hii ya kudhalilisha watu imeshika kasi na utetezi wenu ni kuwa anatania. Jee na yeye tumtanie atakaa kimya?
Wengine huwa hawataniwi bana
 
Huwezi kuleta utani ambao ni matusi mbele ya hadhira. Kwa maana halisi, mwanamke anayegombea wanaume ni KAHABA au MALAYA. Jee Jokate anagombea wanaume?

Jee Jokate ni Malaya au Kahaba kulingana na maneno ya Rais?

Tabia hii ya kudhalilisha watu imeshika kasi na utetezi wenu ni kuwa anatania. Je, na yeye tumtanie atakaa kimya?
Siyo kukaa kimya tu.....

Bali wengine wako jela saa hizi kutokana tu na kumtania Mheshimiwa Rais

Refer kesi ya Idris, ambaye ameendelea kuteseka kwenye "selo" za Polisi, kwa kile kinachodaiwa kosa la kucheka suti ya Mzee Baba!
 
Mkuu umesoma science nini Tanzania

Umeshindwa kumuelewa Rais

Soma Fasihi, Rais aliongea vitu tofauti na fikra zako

Umechemsha mkuu, Ulisikiliza hotuba au umesimuliwa
Hakuna fasihi kwenye kumvua nguo mtu hadhani.
Alafu kwanini itumike fasihi kwenye majority, wakati siyo wote wanaojua hiyo fasihi?

Wewe ndiye uliyechemsha sana, na nakushauri rudi shule
 
Chonde chonde Rais Magufuli, najua wewe ni vigumu sana kubadilisha kile unachokiamini lakini elewa kuwa sisi sote ni binadamu hivyo kujisitiri na kuwasitiri wenzetu ni jambo la muhimu kweli kweli.

Na hili linachagizwa zaidi na pale unapoamua kuwavua utu hao wasaidizi wako kisha na wao wanafurahia na wengine kwa kupiga makofi kabisa. Kwenye nchi za watu waliostaaribika, waisoendekeza njaa na dhiki kwenye vyeo ungeona tofauti kubwa sana na pengine tabia hii ingekoma mara moja.

Sina shida na wewe kumsema DC wa Kisarawe kuwa anagombea wanaume. Hilo ni lako na yeye na kwa jinsi alivyoonyesha reactions shauri yake! Ni muendelezo uleule wa watu kudhalilishwa na wao badala ya kuonyesha kuchukizwa na udhalilishwaji huo wanaishia kufurahi na kupiga makofi eti kwa kuwa ni Rais kasema. Hii imejenga picha mbaya hata kwa wasaidizi wako na wao kuwadhalilisha wasaidizi wao kimamlaka hadharani.

Shida yangu kubwa ni wewe kumpeleka moja kwa moja mteule wako mpya wa u-DAS kwenye shutuma hizo hizo akiwa hata bado hajaanza kazi. Yani ujumbe wa moja kwa moja uliompa ni kuhusu kugombea wanaume. Hii si sawa hata kidogo.

Kama uliona tatizo hilo lipo kwa DC wa Kisarawe basi ilitosha kabisa kumuonya yeye kama yeye na siyo kumuhusisha na mtu mwingine ambaye kimsingi ndiyo kwanza anaanza majukumu mapya.

Rais, kumbuka kuwa kwa sasa kuna teknolojia pana ya utafutaji taarifa na inamilikiwa na watu wengi sana. Matamshi yako yatadumu kusikilizwa kwa vizazi vingi vijavyo hivyo inakupasa kuwa na uangalifu mkubwa.

Aidha, Jokate kimsingi amepewa hati chafu na huenda sasa hata afanye nini bado ataonekana ana sifa mbaya ya kugombea wanaume ofisini. Hii ni sifa mbaya na ya mwisho kwa mwanamke! Mbaya zaidi imetolewa na Rais tena hadharani.
Magufuli,Jokate,Kisarawe,CCM,serikali,blah blah blah...

Yaani hiyo lineup hapo juu,I better go into my toilet and shit all day!
 
Tafadhali, tuwekee na video clip.
 
Ni kweli kabisa. Yale matamshi hayakua ya kiungwana kabisa ni udhalilishaji. Na wale kenge wa kijani wakampgia makofi.
Nadhani wewe ndiye umedhalilisha wenzio kabisa. Kama unadiriki kuwaita wenzio kenge, then sioni uhalali wa kuwatuhumu wengine juu ya tabia ya udhalilishaji.
 
Sasa kama Jokate anagombea wanaume ofisini kwanini huyo Mtela akatumbuliwa kwa kutongoza wake za watu? binafsi naona wote wana sifa zinazofanana tofauti yao jinsia tu.
Huyo jamaa amemtongoza DC au? Jiwe hatakagi kufuatwafatwa
 
mtoa mada sikuungi mkono acha kumsingizia jiwe ila inaitwa majazi utani ndani yake
 
DAS mtumbuliwa alileta utani mtaniwa akamuonya mara kadhaa hakusikia

kaishia kupotea, Mkubwa hataniwi
Huwezi kuleta utani ambao ni matusi mbele ya hadhira. Kwa maana halisi, mwanamke anayegombea wanaume ni KAHABA au MALAYA. Jee Jokate anagombea wanaume?

Jee Jokate ni Malaya au Kahaba kulingana na maneno ya Rais?

Tabia hii ya kudhalilisha watu imeshika kasi na utetezi wenu ni kuwa anatania. Je, na yeye tumtanie atakaa kimya?
 
Tatizo letu ni ajira unafikiri ni kuendeleza njaa? mtu ata atukaniwe mama yake mzazi atachekele na kupiga makofi ili mradi anabaki kwenye ajira
Tena wakitaitiwa ndo wanatoa sifa za kupitilia eg Mzee wa miuno Kangi alipofurumushwa ofisini na kufunguliwa mashtaka na baadaye kuonekana na hatia ameishia kumfananisha Magu na utatu mtakatifu kwamba alizaliwa pasipo na dhambi (Yesu Kristo) na baadaye na kuongeza kuwa 'Yeye ndiye aliyeniteua na sasa amaetwaa uteuzi wake jina la Magufuli lihimidiwe'.
 
Mke wa mtu sumu na Chakula ya Mkubwa ni Kombora, ukilichezea litakulipukia

DAS mtu mdogo sana lakin unapata bahati ya kukanywa na Amiri jeshi lakin husikii mpaka anakufukuza
Wakuu huwa ninamshukuru sana Mungu kwa hatua aliyonifikisha kimaisha. Nashauri pambana uwe boss wewe mwenyewe katikaka biashara yako hata kama ni ndogo. Hata ukiwa umeajiriwa fanya kamradi kaziada ambacho wewe ni boss na ninakuhakikishia hutataka vyeo vya kupewa na kunyang'anywa kwa kuwa kwanza hutavipenda maana vitakufanya busy ushindwe kufuatilia deal zako. Wanasema cha kupewa si Chako ni kama cha kuazima hakisitiri ma ta ko.
 
Wewe nae pumba tu, huoni maana ya kugombania wanaume ni kupenda kulalwa, sasa hii inasema hadharani utani gani huo?

Mwanao akikwambia baba au mama unagombania wanaume au wanawake mbele ya familia utasema utani? Lumumba kama hamna akili kabisa basi jilazimisheni kuwa nayo hata kidogo kwa kunyamaza.

Maana kwa comment yako hata zezeta anaonekana ana akili maana japo anavuja mate kakini amekaa kimya
Toka lini Lumumba wakawa na akili? ktk utawala huu hakuna msamiati walonao zaidi ya sifa na mapambio hata kama ulioongelewa ni upuuzi lazima wausifie, mbaya zaidi kama aleongea na mzee baba hizo sentensi zitasafishwa na Bulldozzer
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom