MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Magazeti ya leo yamejaa habari inayosema Serikali ya Magufuli yuko mbioni kuleta mswaada wa sheria utakaotenganisha siasa na biashara.
Wabunge watakuwa na sheria inayowazuia kuwa wafanyabiashara ambapo pia wafanyabiashara hawataruhusiwa kuwa wabunge.
Vivyo hivyo itakuwa kwa madiwani mpaka wenyeviti wa vijiji na mitaa.
Baadhi ya wabunge wamepinga mswaada huo huku wakidai pesa za ubunge hazitoshi na ndio maana wanaamua kuwa na biashara ili kukabiliana na hali za kimaisha.
Wabunge wengine wamesema hawawezi kutoa maoni yao mpaka wausome huo mswaada.
Inasemekana Rais Magufuli amewaambia wabunge wa CCM wana uhuru wa kuchagua kama wanataka wawe wabunge au wafanyabiashara.
Tume ya Maadili itapewa meno na nyenzo za utendaji ili iweze kufanya uchunguzi wa kina kwa kila anayejaza fomu za maadili na Itakuwa ni kosa la jinai lenye adhabu kali kudanganya katika fomu za tamko la mali.
===================
Sheria yaja kutenga siasa, biashara
job ndugai*Tume ya maadili kupeleka muswada bungeni
*Wabunge wapinga,wasema wanalipwa kidogo
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewatangazia wabunge kuwa Tume ya Maadili na Utumishi wa Umma inatarajia kupeleka muswada wa sheria bungeni kwa ajili ya kutenganisha biashara na uongozi.
Ndugai, alitoa kauli hiyo Dodoma jana alipozungumza kwenye semina ya kwanza ya wabunge wanachama wa Chama cha Wabunge Wanaopambana Rushwa (APNAC) katika Bunge la 11.
“Ninaomba niwaarifu jambo muhimu na ninaomba mnisikilize kwa makini. Nimepata ujumbe kutoka Tume ya Maadili na Utumishi wa Umma inayoongozwa na Jaji Salome Kaganda kwamba wana nia ya kuleta muswada wa sheria bungeni wa kutenganisha uongozi na biashara.
“Muda si mrefu nitawaalika waje watoe semina au watoe maelezo kwa wabunge wote muweze kuielewa vizuri.
“Sasa wale wenzangu ambao ni wavivu kusoma, wasome sheria hiyo na kuielewa kwa sababu ubunge wetu tunauchanganya na biashara ili mambo yaende sawasawa.
“Wale ambao tumezoea kusema ndiyoo…naomba sheria hii ikija muisome kwa makini na muelewe maana wengi wetu wabunge tumekuwa tukichanganya na biashara ili kuweka mambo sawasawa.
“Unaweza kupitisha sheria halafu ukaendelea na biashara, hapo utakuwa umejiweka pabaya,”alisema.
Aliwatahadharisha wabunge ambao wamekuwa wakiunga mkono na kupitisha sheria mbalimbali kuwa makini kuhusu sheria hiyo.
Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM), alisema katika nchi zilizoendelea imekuwa ni kawaida mfanyabiashara anapokuwa mbunge anakabidhi biashara kwa mtu mwingine.
“Nchi zilizoendelea unakabidhi biashara kwa mtu halafu unaendelea na ubunge lakini sisi hapa kwetu imekuwa ngumu. Hivyo naomba msome hiyo sheria vizuri tuielewe. Ni sheria nzuri kwa sababu malengo yake ni mazuri.
“Sasa sisi waswahili tulivyo… kumkabidhi mtu biashara yako kwa miaka mitano ni jambo gumu na baada ya miaka hiyo mitano kuisha unaweza ukaendelea mpaka 20 ukiwa bungeni hivyo kukaa miaka yote halafu unarudi unamwambia aah mzee vipi biashara yangu imefikia wapi hapo,”alisema.
Aliwaasa wabunge kuwa makini na vishawishi vya rushwa na kwa vile nafasi zao ni nyeti wafanye kazi kwa unyoofu.
“Nafasi tulizonazo ni nyeti, kwa mwenendo wa Serikali ya awamu ya tano yawezekana kabisa wakawapo watu ambao wanaona umakini huu maslahi yao na hivyo wakaona njia pekee ni kuwarubuni, nawaasa msishawishike,”alisema Ndugai.
Aliwataka kuwa mfano katika jamii kwa kudhibiti rushwa kwa kuwa wabunge ndiyo wanaopitisha sheria mbalimbali.
“Mna wajibu wa kudhibiti rushwa na kuwa mfano katika jamii na mna jukumu la kupitisha sheria ya kupiga vita rushwa kwa miswada inayopita bungeni.
“Mnavyopitisha bajeti ya serikali mhakikishe vyombo vinavyopambana dhidi ya rushwa vinatengewa bajeti ya kutosha,”alisema Ndugai.
Alimkumbusha Waziri wa Utawala Bora Waziri wa Ofisi ya Rais,Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki kuwa wabunge wanakumbwa na ukata mkubwa hivyo Serikali iwaangalie kutokana na majukumu waliyonayo.
“Najua mna pressure kutoka kwa wananchi kuwapa fedha, kuchangia harusi, misiba, kununua madawati, kulipa ada ya wanafunzi hivyo kutokana na hilo mnajikuta ni hohehahe na inabidi sasa ahangaike huku na kule na baadaye kujikuta anaingia kwenye kona mbaya.
“Tatizo jingine ni mikopo ya benki yenye riba kubwa nayo inawasumbua sana wabunge wangu na inawaweka katika mazingira magumu.Naomba hili pia litazamwe.
“Pia ukata kwa ujumla wake na waziri uko hapa…naomba nikwambie kwamba wabunge hawa hawako vizuri, kuna haja ya kuweka mambo yao vizuri. Maana huwezi ukampa mtu madaraka halafu mfukoni hana kitu na ana majukumu mazito,”alisema.
Waziri Kairuki aliwataka wabunge kuwa sehemu ya kupambana na rushwa na kila mmoja kwa nafasi yake awe msafi.
“Ifike wakati hata tusilaumiwe kwa sababu kitendo cha kutumiwa tu inaleta shaka. Hivyo chombo hiki kiendelee kuchangia mapambano ya rushwa na tutaleta sheria bungeni,”alisema Kairuki.
Alisema adhabu ambayo inatolewa kwa wahusika haiendani na hasara ambayo taifa linapata.
“Kama serikali tutahakikisha watoa taarifa tunawalinda na tutahakikisha TAKUKURU inakuwa huru,”alisema.
Akitoa mada katika semina hiyo, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Davis alisema bado rushwa ni tatizo nchini kwa kuwa inafanywa kwa usiri.
“Rushwa ni makubaliano kati mpokeaji na mtoaji hivyo ni ngumu kuwabaini na rushwa kubwa inafanywa na wanasiasa na wale wenye uwezo wa uchumi,”alisema.
Alisema adhabu ya wale wanaokamatwa na rushwa bado ni ndogo na imekuwa ikilalamikiwa kwa sababu haiendani na kosa.
“Na rushwa kama haijaondoka kwenye mawazo ya mtu hata tukiwa na sheria ni bure. Cha kufanya ni lazima lianzie kwa wabunge wenyewe na tusiwe na ujasiri wa kuwanyooshea vidole wengine bali tujiangalie wenyewe kwanza,”alisema.
Akichangia mada katika semina hiyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM) alisema ni kesi nyingi za mafisadi ambazo zimelepekwa mahakamani lakini wanapewa muda mchache.
“Mshahara wa mtu unajulikana, halafu mnasema kukamata rushwa kubwa ni ngumu, itungwe sheria ajieleze hizo mali kapata wapi.
“Na wako ambao wamepelekwa mahakamani lakini kesi za wengine haijulikani zinaishia wapi kwa sababu wengine wanahonga.
“Hivyo kinachotakiwa kutungwa sheria, aitwe ajieleze akishindwa kujieleza anyang’anywe mali zake na apelekwe jela,”alisema Keissy.
MAONI YA WABUNGE
Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM), alisema kitendo cha kutenganisha biashara na uongozi kwa wabunge ni ngumu kwa sababu mishahara na marupurupu yao madogo.
“Kwa nchi yetu haiwezekani. Kwa sababu ukiangalia mishahara, marupupu kwa nchi hizi za Afrika Mashariki (EAC) Tanzania ni ya mwisho. Ukizungumza hivyo mtu asiwe na kitu chochote cha kumwingizia kipato ni ngumu na haiwezekani.
“Mfano; mshahara wa mbunge wa Kenya uko zaidi ya mara 10 ya mbunge wa Tanzania na bado anafanya kazi zake. Mbunge ni mtu ambaye hayuko juu ya sheria ingawa anatunga sheria,”alisema Shabiby.
Aeshi Hillaly
Naye Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillaly alisema kwa hali ilivyo hivi sasa, ni vigumu kumtenganisha mbunge na biashara na ni jambo lisilowezekana.
Paresso
Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso (Chadema), alisema hajajua maudhui ya muswada huo hivyo akiusoma ndiyo atajua.
“Uletwe tuusome lakini ni vigumu kwa hali ya sasa kumtenganisha mbunge na biashara,”alisema.
Kikwete
Mwaka 2008, Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza alitangaza kutenganisha siasa na biashara.
Alisema upo ushahidi wa migongano ya maslahi kwa baadhi ya wabunge na mawaziri ambao ni wafanyabiashara na wanasiasa, jambo ambalo huweka katika mazingira magumu ya utendaji.
“Nchi za wenzetu hasa zile za kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizi… taratibu unaomtaka mtu mwenye shughuli za biashara anapokuwa mbunge au waziri kuacha kujishughulisha na biashara zake.
“Unakuwapo utaratibu rasmi unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye kujihusisha nazo. “Anapoacha uongozi wa siasa kama atapenda atachukua tena mali yake na kuendelea na shughuli zake.
“Ni makusudio yangu kuwa utaratibu huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au ubunge na uwaziri.
“Kwa ajili hiyo ni makusudio yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi ili tuingize utaratibu huo,”alisema Kikwete.
Alisema ni jambo lenye maslahi kwa taifa na litasaidia kujenga heshima ya viongozi wa umma mbele ya macho ya wananchi.
Chanzo: Mtanzania