Rais Magufuli: Kukaa hapa kwenye nafasi hii nimechoka kweli, kazi hii ni mateso, unaweza kujiuliza haya ni maisha gani, maisha haya ni magumu

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
46,676
71,034
Viherehere wote chalii wameaibika sura zimewafubaa kujipendekeza kumekwisha

Watu walikuwa wanajirusha fahamu lakini wameshushuliwa sijui wataingiza wapi sura zao

Mungu ni mwema Mungu ni mwema.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa chama hicho ni kiwanda kinachopika viongozi bora, hivyo hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kinyume na Katiba ya chama hicho na Katiba ya nchi.

Mhe. Rais Magufuli amesema majukumu ya Urais ni mazito na kwamba hata yeye hakutarajia kama angekutana na uzito wa majukumu anaokutana nao hivi sasa.

Ametoa kauli hiyo alikuwa akizungumza katika vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyofanyika Jijini Mwanza.

"Kukaa hapa kwenye nafasi hii nimechoka kweli,kazi hii ni mateso, unaweza kujiuliza haya ni maisha gani, maisha haya ni magumu kazi hii ni ngumu,mimi sikujua kama ni mateso,lakini nimeipata,halafu kila msalaba,kila tatizo lazima lije kwako".Rais Magufuli.

Mwaga manyanga mzee kweni umeandikiwa na Daktari
 
IMG-20191215-WA0005.jpg

Hahaaa ,Mzee ananyonya tu so anaweza kusema lolote.
 
Wakuu hamjambo?

Kauli ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JJPM kuwa urais ni kazi ngumu huku akisema kuwa hakujua kuwa kazi hiyo ni ngumu hakika inatuuumiza sana sisi wazalendo ambao bado tunaimani naye kwa 100% huku ikiwapa nguvu mafisadi kuwa wakiongeza juhudi wanao uwezo wa kumfanya akate tamaa na hivyo wawe huru kuiba pesa za uma na kuihujumu nchi.

Naomba mh utambue kuwa wewe ndiye Mussa ambaye umepewa nafasi ya kutupeleka kanani inchi ya ahadi na dalili tunaziona kuwa tumekaribia kufika ,sasa kama wewe ndiye uko mbele na unayaona yaliyoko mbele basi tupe moyo kuwa uko pamoja nasi na utatufikisha Kanani.

Naomba nikili wazi kuwa ikiwa mwalimu anayeaminiwa na mwanafunzi wake ataanza kusema somo analofundisha ni gumu ,basi wanafunzi watakata tamaa na kushindwa kufaulu somo hilo,


Jpm piga kazi ,2020 huna mpinzani,Mungu awe nawe daima.

Mheshimiwa rais najua kuwa kuongoza ni kazi ngumu ila jipe moyo,wa Tanzania bado wanaimani na wewe,na ndio maana kila uchwao wanapigana ili katiba ibadilishwe ili uweze kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi wakiamini kuwa kazi yako ni nzuri,mheshimiwa rais piga kazi bado tukuamini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kazi ya urais ni ngumu ila sio ugumu anaousema yeye. Sehemu kubwa inayomfanya aone ugumu wa ajabu kwenye hiyo kazi ni yeye kutaka kuhozi kila kitu, huku akiikataa katiba mpya ambayo ingetoa mamlaka makubwa kwenye mifumo kuliko mtu. Ni sawa na mtu kusema kazi ya kilimo ni ngumu, lakini hataki kutumia tractor bali analazimisha kulima kwa jembe la mkono!

Kitendo cha yeye kuona anafanya kazi ya urais kama ya kujitolea na sio jukumu ambalo analipwa mshahara, ndio kunamfanya aone hiyo kazi ni ngumu, jambo ambalo sio kweli. Aheshimu box la kura tuone kweli anamaanisha kuwa hiyo kazi ni ngumu, sio unanajisi box la kura ili ww na chama chako muendelee kuwa madarakani kwa njia haramu, kisha useme hiyo kazi ni ngumu, hatudanganyiki.
 
Historia inaonyesha kua Hitler si yeye aliyetaka kufanya awe msujudiwa badala yake ni officials wengine kabisa. Ilikua mtumishi wa umma anakula kiapo kwa kuahidi kuitumikia Ujerumani, hawa officials wakajipendekeza na kubadilisha kiapo na kikawa kinasema unaahidi kumtumikia Hitler.

Hata Nyerere aliwahi sema kua alikua anaambiwa subiri kidogo usiachie madaraka mambo hayajawa tayari.

Nahisi ni same hata kwa Magufuli. Yeye hana mpango lakini wapambe ndiyo wapo bize kutaka hilo lifanikiwe, likifanikiwa miaka 10, 25 mbele atakayegewa lawama ya uroho wa madaraka ni Magufuli, siyo Nkamia wala Pinda.
 
Hizi ni Hadithi ya Sungura Mjanja" SIZITAKI MBICHI HIZI" madaraka matamu sana Mkuu. Atakujasema nilikuwa sihitaji hata kuongeza duru ya pili lkn Watz Wanyonge wamenililia basi nami kwa huruma za kibindamu nikaona nikubali kuongeza angalau miaka mingine kadhaa. Niomba muniombee nami namtanguriza Mungu ili anisaidie kuubeba huu msalaba wa hawa Watz masikini walioteswa kwa miaka mingi kwenye awamu zilizopita.
 
Mafisadi wakiskia kauli kama hizi wanapata raha sana maana kwao ni afueni mzee akichoka na kulegeza juhudi za kuwabana, rais tunakuombea, wewe ni mfano wa kuigwa Afrika yote.
 
digba sowey, Watz wepi hao Mkuu? Huku mtaani kwetu hawataki hata kuona picha yake kwenye Tv. Labda wewe unawazungumzia lile kundi dogo la wanufaikaji.

Leo hii Wanafunzi wa Elimu ya juu wanataabika hawajapata mikopo yapata mwezi na ushee sasa. Wakulima wa Korosho hadi leo malipo yao yanafanyiwa uhakiki. Maduka ya kubadilishia fedha za kigeni hadi leo hawajui hatma ya fedha zao na mahakamani hawapelekwi. Wewe huna tofauti na mwanaume anaemlaghai mwanamke mgumba kuwa mwaka huu ni wako lazima unyonyeshe mtoto.
 
Back
Top Bottom