Rais Magufuli kuhusiana na Corona bora ukachukua hatua bila kuchelewa zaidi unauweka uongozi wako njia panda

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
MODs natumaini mtaunusuru uzi huu kumwangazia mheshimiwa rais hali ilivyo, ili naye, aweze:

1. Kujinusuru mwenyewe kuweza kuendelea kuongoza kama kazi hiyo anaipenda.
2. Kuyanusuru maisha ya watu wake wasio na hatia kwa maana ndiyo kazi kuu tuliyompa kama rais wetu.
3. Kulinusuru taifa ili hatimaye liweze kusimama tena na hata kuendelea na jitihada za kujijenga kama sehemu ya maisha anayowajibika kuyasimamia yeye kama rais.

Nikiazima maneno ya rais Kenyatta jana: "Siwezi kuyaweka maisha ya wakenya hatarini kwa kulinda uchumi usiangamie". Mwisho wa kumnukuu. Maneno ya busara kabisa ambayo tunahitaji kuyasikia pia kutoka kwa rais wetu.

Mheshimiwa rais, kwa uamuzi uliochukua wa kulinda uchumi dhidi ya maisha ya watu, kwa hakika utakuwa unajielekeza kubaya. Kwa maneno yako mwenyewe ulisema: "mtanzania wa leo si yule wa jana". Mwisho wa kukunukuu.

Kwamba hatuelewi nini maana ya haya Mabuti, mabarakoa yote haya, mazishi kufanywa na serikali, kuhudhuriwa na watu 10, 10? Nk nk?

IMG_20200428_175237_033.jpg


Yapo mawazo kuwa mmechagua wanachoita "the devil's alternative". Mmechagua shetani awatangulie. Uchumi, yaani fedha mmezitanguliza mbele. Katika dilemma ya nini kilindwe mwanzo: uchumi au maisha, mmechagua kulinda uchumi na kuwa wa kufa acha afe wa kupona acha apone.

Kete mmeielekeza zaidi kwenye kutegemea chanjo au tiba ukisali mchana na usiku, beberu aipate mapema kadri iwezekanavyo. Kwa ufupi, umechagua kusubiria kuokota embe dodo chini ya mnazi.

Wakati ukifanya hivyo, mmejikita katika propaganda zaidi ili kununua muda. Uchaguzi mkuu 2020, sala za kuombea taifa nk zote ni propaganda zako. Kwa hakika propaganda hizi hazitakusaidia.

Zaidi ya yote inafahamika kuwa wale watu watu wako wapo pote kwa ajili ya propaganda na kuleta mitafaruku kwenye suala hili kadri iwezekanavyo. Wamekuwa mabingwa wa kuwachagiza wenye mawazo mbadala ati kuwa waihame nchi. Wamekuwa wenye kushadadia kuwa nchi hii haina uwezo wa kuwalisha watu wake wakati nchi maskini kuliko sisi zimeweza kuhimili masuala ya njaa kwenye vita hivi muhimu kwa kutumia raslimali zao. Wananchi wao wameweza kumudu kuishi katika muda huu mgumu (lakini muhimu) wa mapambano na ugonjwa huu.

Watu wako hao hawana hoja zaidi ya kudhani wanaweza kirahisi rahisi kutuaminisha ati kuwa hata matukio mageni ya vifo vingi hivi vya ghafla yakiwamo majina mazito mazito ati kuwa ni mambo la kawaida yatokanayo na magonjwa ya kawaida.

Hata hivyo ukweli unabakia wazi, huo uchumi unaolinda tayari umekwama mno. Ni sekta ipi inayofanya vizuri sasa hivi? Ni sekta ya utalii, usafirishaji, usafiri wa umna, mahoteli, michezo, ujenzi, elimu? Ni ipi ina nafuu? Haipo.

Na bado, kwani wakati maambukizi yanazidi kuwa makubwa zaidi, vifo vinaongezeka na wagonjwa wanaongezeka. Tayari majirani zetu hawaoni tofauti yetu na Corona. Si muda mrefu watatususa na ndipo yale makaa unayojipalia yatakapokukabili vilivyo.

Kwa hakika haikuhitajika elimu kubwa kuweza kuona maisha yalipaswa kulindwa kwanza. Tulikuwa nao uwezo kama taifa kuudhibiti ugonjwa huu.

Hata hivyo mkuu, bado ungalipo. Mtanzania ni mwenye kusamehe sana. Kila siku husema: "yaliyopita si ndwele". Bado unaweza kurekebisha mambo hata sasa na tukakuunga mkono tu. Wanasema "better late than never" au "chelewa ufike".

Kukunong'oneza mkuu, vifo hivi vya ghafla ghafla kwa wingi huu, wengi wetu na wewe ukiwamo, tunajua vinatokana na nini. Mbaya zaidi, sote kabisa na wewe ukiwamo tunajua pia - tulikuwa na uwezo wa kuvizuia.

Leo vifo hivi vimetokea kwa hawa, kesho watakuwa wale na kesho kutwa waleeee! Waathirika wanazidi kuwa wengi.

Wasikudanganye, kwa status quo: "unajipalia makaa mkuu".
 
Nani wa kumfunga Paka kengele?

Wale watu wake wa propaganda hawapendi kusikia hili: "ngoja lichanganye".

Nani asiyejua litachanganya? Kama hatua hazichukuliwi ni lazima lichanganye na hapo ndipo penye kujipalia makaa.

Karata nyingine ya wapiga propaganda ni kuhusu vifo: "kwani mlitaka vifo viwe vingapi?" Kana kwamba wao wana majibu ya kuwa "hawakutaka viwe vingapi?"

Ni suala la muda tu.
 
Wale watu wake wa propaganda hawapendi kusikia hili: "ngoja lichanganye".

Nani asiyejua litachanganya? Kama hatua hazichukuliwi ni lazima lichanganye na hapo ndipo penye kujipalia makaa.

Karata nyingine ya wapiga propaganda ni kuwa ni kuhusu vifo: "kwani mlitaka vifo viwe vingapi" kana kwamba wao wana majibu ya kuwa "hawakutaka viwe vingapi".

Ni suala la muda tu.

Lichanganye mara ngapi mkuu? Hali sio hali tena
 
Lichanganye mara ngapi mkuu? Hali sio hali tena

Hapo unapoliona hali ni mbaya lakini bado halijachanganya sawa sawa.

Mkuu wataalamu wanasema kwa Africa bado hatujafika peak.

Likifika peak hapo ndiyo sasa litakuwa limechanganya vilivyo.

Na hicho ndicho kipindi ambacho majoka yote bila kujali yalipo itabidi kutoka mapangoni.
 
Back
Top Bottom