Rais Magufuli kuhamia Dodoma kabla ya Disemba Mwaka Jana

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,788
106,421
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa alisema Rais John Magufuli kuhamia Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma wakati wowote kabla ya Desemba mwaka jana

Majaliwa alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Jiji la Dodoma katika kilele cha ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi.

"Hakuna kitakachokwamisha. Makamu wa Rais yupo Dodoma na mimi nipo Dodoma hivyo amebaki Rais. Leo niwaambie kuwa atahamia wakati wowote kabla ya Desemba 30 mwaka huu," alisema Majaliwa.

My Take
Ahadi bado ipo palepale JPM atahamia Dodoma kabla ya December 2018 licha ya sasa kuwa ni March 2019.

Credit Asprin
 
Kitu ninachowapendea ukoo wa CCM, huwa wanajua kutoa vikauli wakiwa na moyo wa kujiamini na visipotimia au kutekelezwa wanajikausha kizima kana kwamba sio wao waliovitoa. Na wanaamini kuwa waTz ni wajinga sana, japokuwa m/kiti wa ukoo juzi alikejeli kuwa 'si wajinga sana'.
 
Ndugu zangu wanaufipa fanyeni kazi majimbon kwenu, kumsema Rais tena kwa vitu ambavyo havina mashiko ni kupoteza mda

Mfano Rais asipo hamia Dodoma sisi wananchi tunapata hasara gani, kwann msiongelee vitu vingine

Siasa sio kupinga tu kila kitu, na mbaya zaidi mda mwingine munaombea kabisa serikali ikosee.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Ndugu zangu wanaufipa fanyeni kazi majimbon kwenu, kumsema Rais tena kwa vitu ambavyo havina mashiko ni kupoteza mda

Mfano Rais asipo hamia Dodoma sisi wananchi tunapata hasara gani, kwann msiongelee vitu vingine

Siasa sio kupinga tu kila kitu, na mbaya zaidi mda mwingine munaombea kabisa serikali ikosee.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kazi yetu ni kupoteza muda
 
Mzee rais kuhama kuna taratibu nyingi, si sawa na mtu kubeba vitu vyake kwenye kirikuu na kuhamia nyumba nyingine. Ulishajiuliza kwa nini mnatangaziwa rais atawasili saa 3 asubuhi badala yake akawasili saa 6 mchana? au ndo ilimradi na wewe uanzishe mada
 
Mzee rais kuhama kuna taratibu nyingi, si sawa na mtu kubeba vitu vyake kwenye kirikuu na kuhamia nyumba nyingine.
Wakati anatangaza kuhamia Dodoma hakuzijua hizo taratibu?

Ulishajiuliza kwa nini mnatangaziwa rais atawasili saa 3 asubuhi badala yake akawasili saa 6 mchana? au ndo ilimradi na wewe uanzishe mada
HIzi ni tabia za kishoshalisti na kwa viongozi wasiojali muda na maslahi ya wananchi wao.
 
Back
Top Bottom