Rais Magufuli kufanya ziara ya kikazi Dar kuanzia Februari 24

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo Katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema ziara hiyo itaanza Jumatano ya February 24 ambapo Rais Dkt. Magufuli atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na Mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

Aidha RC Kunenge amesema Siku ya Alhamis ya February 25 Rais Dkt. Magufuli ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 Asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambapo Kuna Studio za Channel Ten na Uhuru FM.

RC Kunenge amesema Siku ya Ijumaa ya February 26 Mhe. Rais atafanya shughuli ya uzinduzi wa Majengo ya chuo Cha Polisi na Kiwanda Cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika Saa 03:30 asubuhi.

Chanzo: IPP Media
 
Huyu bwana lazima atakuwa ana matatizo makubwa ya akili maana haiwezekani viongozi wenzake Dunia nzima wanakwepa mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ila yeye anakwenda kukusanya watu kuzindua mpaka vyoo vya stand.
Mkuu unaelewa maana ya KISIWAGA? KIKWETU HILO JINA DAAAAAH, USINGEJIITA KABISA.
 
Huyu bwana lazima atakuwa ana matatizo makubwa ya akili maana haiwezekani viongozi wenzake Dunia nzima wanakwepa mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ila yeye anakwenda kukusanya watu kuzindua mpaka vyoo vya stand.
Dah, kuna Saccos zinawaharibu akili wafuasi wao. Haiwezekani mkuu akitulia zake Chato wanaimba kajificha...! Akiamua achape kazi watakuja na maoni kama ya Huyu mja hapa....which is which. Kipi kizuri kwenu nyie watu?
 
Dah,....Kuna Saccos zinawaharibu akili wafuasi wao....Haiwezekani mkuu akitulia zake Chato wanaimba kajificha...! Akiamua achape kazi watakuja na maoni kama ya Huyu mja hapa....which is which....Kipi kizuri kwenu nyie watu?
Huyu Mungu wa Kabudi tutamsakama mpaka akimbilie kwenye sayari ya Mars
 
itakuwa vizuri endapo latra nao watampa maelezo kwanini tukatiwe ticket kwa system ya. p.0.s na sio kwa mashine za efd kitu ambacho kimeongeza kiwango cha nauli za bus kwa wasafiri wote.

Wamweleze huyu dalali anayejikita katikati ya bus owners na tra ni nani na kwanini uwepo wake ubebwe na wanyonge wa kiuchumi?
 
Dah,....Kuna Saccos zinawaharibu akili wafuasi wao....Haiwezekani mkuu akitulia zake Chato wanaimba kajificha...! Akiamua achape kazi watakuja na maoni kama ya Huyu mja hapa....which is which....Kipi kizuri kwenu nyie watu?
Kizuri kwao ni upigwamiti tu. Kwenye uchaguzi yule 'lafa' wao kaja na ajenda ya ushogeshwaji wakakimbilia kuunga mkono bila hata kuchanganya na zao!
 
Back
Top Bottom