Rais Magufuli kufanya kikao maalum leo na Mawaziri, Makatibu, MaRCs, MaRAS na TRA

Status
Not open for further replies.
tunamkumbusha hasisahau kutoa maagizo kwamba,wastaafu walipwe pesa zao mara moja maana wanateseka sana,hivi ni kazi gani nyigine ya muhimu inayofanywa na hiyo mifuko zaidi ya kuwalipa wastaafu pesa zao?
 
tunaelekea mwaka wa nne saivi lakin bado hajapanga safu yake ya uongozi sasa mzee anatapatapa


SMART

S= Specific (Hayuko specific anataka nini, Mara kahamia Dodoma, Mara Kajenga uwanja wa ndege Chato, Mara Kanunua Bombadia, Mara Stieglers, Mara SGR)-Alitakiwa achague mradi mmoja mkubwa, maximum miwili tu basi adeal nayo hiyohiyo mpaka kieleweke

M=Measurable (Kwa kuhamia Dodoma anapimaje mafanikio yake kwa mfano, Je kuhamia Dodoma kunaongeza nini katika uchumi?)

A =Attainable (Je ana hela za Kuattain kila Mradi?)
R=Relevant (Je midege ni relevant?, Kuhamia Dodoma ni relevant?, Kurudia rudia chaguzi ndogo bila sababu za msingi ni relevant?)

T=Timely (Yuko tayari hiyo miradi imaliziwe na watakaomfuata, au anataka ndani ya miaka yake miwili au saba iliyobaki iwe imekamilika?, Je yuko tayari tule Nyasi ili ambition yake hii ifanikiwe?)

Akitaka kuachieve ambition zake, ana option moja tu nayo ni KUKUZA UCHUMI, BILA KUKUZA UCHUMI WATU WANAWEZA KUTAMANI KUGEUZA RELI YA SGR SCREPA WAKAUZE WAPATE HELA YA KULA!, Achana na njaa aisee!!!
 
Rais Magufuli leo katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam atafanya kikao maalum na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa(RAS), BOT na watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA). Hiki ni kikao maalum kinachohusu wasimamia sera serikalini.

Kikao hiki ni maalum kwa ajili ya utendaji wa kazi kwenye eneo la ukusanyaji wa mapato na uthibiti wa biashara ya fedha nchini na ubora wa bidhaa nchini.

Ikumbukwe kuwa katika uchunguzi uliofanywa na IMF mwezi uliopita ilibainika kuna udhaifu mkubwa katika udhibiti wa biashara ya fedha za kigeni nchini.

IMF executive board iliishauri serikali ihakikishe inadhibiti vizuri biashara ya fedha za kigeni nchini.

Ushauri wa IMF executive board ni huu;
Directors emphasized the need to enhance surveillance and monitoring of liquidity risks in foreign exchange, and introduce regulations aimed at limiting them. These regulations, buttressed by macroprudential requirements, would complement measures to promote proactive foreign exchange risk management by banks and corporates. Completing operational guidance for emergency liquidity assistance, including in foreign exchange, also remains a priority.

Ikumbukwe Nov 19 serikali ilifanya operesheni katika maduka ya kubadilisha pesa za kigeni katika Jiji la Arusha.

LINK>>>Serikali yazifungia benki tano kuuza na kununua dola

Kama una macho na masikio, sogea kwenye Luninga ili upate kile ambacho kitajadiliwa na kutolewa uamuzi na wasimamia sera serikalini.

Ratiba ya kikao kama ifuatavyo;
DuAHto7WsBA092y.jpg:large
Huu ni upotoshaji mkubwa wa tafsiri,IMF haijasema kuna udhaifu mkubwa katika udhibiti wa fedha za kigeni.Usahihi ni kwambaa IMF inasisitiza kuongeza uangalizi/usimamizi/umakini kwa vihatarishi"risks" katika biashara/sekta ya fedha za kigeni nchini.
 
Hivi siku hizi TRA wamekumbwa na nini wasitutolee mapato na matumizi kila mwezi au ndiyo imebumaaa
 
Solution ni moja tu mzee wangu

1. Pangua safu yako ya MaRas na MaDas, uliwaweka kwa kufuata vigezo vya ukada kwa CCM badala ya vigezo vya utaalam, uzoefu etc. Matokeo yake wengi ni poor performers. Kumbuka hawa ndo wana mafungu ya pesa za serikali

2. Toa Tax incentive mzee, punguza import tax za bidhaa mbalimbali, ili kwa sasa watu waagize mzigo ujae nchini.acha biashara zinawiri tena, najua kuwa Exports ni better kiuchumi kuliko import lakini katika hali ya kustabilize tax base yako lazima utengeneze tax payers wa baadae ( Fanya kama alivyofanya mzee Mwinyi )

3. Punguza kodi, lakini Tengeneza mfumo wa serikali kupata stahiki yake bila kupoteza senti. Ili hili lifanikiwe Kwa kuanzia hakikisha kila mtanzania above 18 years ana account ya benki, na tengeneza mfumo rasmi wa ICT wa serikali wa kupata baadhi ya huduma kwa kulipia kupitia mfumo huo, huu mfumo utalink na account ya benk ya mtu hivyo basi serikali itaweza kumonita kila senti ya biashara inayofanyika na hivyo kujua kila senti ya kodi yake itakayokuwa inaingia. Kwa sasa unaweza kuendelea na EFD, lakini EFD ni mfumo butu, huwezi kuumonitor at a real time, Tafuta mfumo mwingine cheaper, robust, easy to use. Unaweza kudesa kwa mifumo ya Wachina ya Wechat Money, Alipay etc. Lakini wa kwetu sharti uwe ni wa serikali na Lazimisha baadhi ya huduma Muhimu watu walipie kwa hii solution!

4. Achana na white elephants projects mzee, Uwanja wa ndege Chato siyo Kipaumbele, Hizo ndege zitakupasua kichwa, jiandae kupeleka ruzuku kubwa tu ya kuliendesha hilo shirika

5. Sisitiza Diplomasia ya Uchumi mzee. Sasa hivi wape mabalozi jukumu la kuwatafuta wawekezaji, na pia kutafuta masoko ya bidhaa zetu hasa za kilimo. Ingia makubaliano na nchi mbalimbali zilizoendelea wakupe quota ya kuuza mazao ya wakulima kwao

6. Usigombane na wanaotusaidia bajeti yetu, yaani wahisani, mambo kama Demokrasia yaache yafanyike, huna haja ya kuwa distracted na uwepo wake, kwa sababu energy kubwa unayotumia kuwaza na kuja na mbinu za kuiminya, ungeitumia kuwaza namna gani uboreshe uchumi mzee wangu tungepiga hatua. by the way una miaka miwili hadi saba ya kukaa madarakani, ni muda mfupi sana, stick na ajenda moja tu uchumi, uchumi, uchumi, Hii ya kuminya upinzani haina maana. Upinzani utakuwepo milele, ukiupunguza nje utaukuta ndani ya CCM

7. Vunja baraza la mawaziri, hawa waliopo akina Mpango wameshindwa kuwa wabunifu wa vyanzo vipya vya mapato, ushauri wao kuhusi fiscal policy hususan ktk miaka ile miwili ya mwanzo ndo umesababisha hali tuliyonayo sasa. Lete sura mpya zenye mawazo mapya

8. Ili upunguze resistance na kelele, na upate kutekeleza ajenda ya maendeleo bila kelele za upinzani, hebu fikiria kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa, ya kamseto fulani hivi ambapo utawaingiza wapinzani ndani ya serikali yako mpige kazi. Kwa kufanya hivi, utapunguza kelele mtaani na pia utaweza kutumia vipaji vingi tu vinavyohitajika kwa ajili ya kuleta maendeleo. Mzee si ulisema maendeleo hayana vyama?
Hizi nondo ni pm nitakuteua kuwa vice- prime minister
 
Missile of the Nation
JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
Pengine umejiunga kwa kazi maalum. Mapendekezo haya ya #kazinabata ndio iliyokuwa practice enzi za Kikwete, nchi haikufika popote, isipokuwa kurudi nyuma. Kupigiwa kelele na wapinzani ni ishara ya kuonesha serikali inafanya vyema. Wapinzani wakikusifia jitilie Mashaka. Tuendelee na #HapakaziTu
Hiv tatizo hua nn vichwan mwenu???
 
Nimesoma ratiba, wataalam 3, NBS,BOT NA TRA,wamepewa nusu SAA kila mmoja, mkuu SAA moja, Kwa kuwa serikali inabana matumizi wangetuma nakala mikoa ni, sioni semina hapo.


Kwani ni semina mbona ni kikao maalum cha...
 
Status
Not open for further replies.
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom