Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,652
Mh.Raisi ninalazimika kutimiza wajibu wangu kama raia mwema kuisemea nchi yangu iokoke kutoka kwenye lindi refu la umaskini,maradhi,ujinga na sasa ufisadi.Kwakua umewafananisha mafisadi na majipu,nawewe ukajipa kazi ya kuyatumbua hayo majipu basi tafuta nyenzo madhubuti ya kutumbulia hayo majipu
- Katiba mpya ambayo hutokana na rasimu ya tume ya mzee Warioba,kwakukubaliana na yaliyomo ndani ya rasimu ile ikiwemo mawaziri kutokua wabunge,kutakua na uwajibikaji wa moja kwa moja kwa mawaziri kwa nafasi zao na wabunge kuwajibika kuishauri na kuisimamia serikali na sio kuisemea/kuitetea serikali kama ilivyo sasa kwa baadhi ya wabunge
- Mbunge asiyetimiza ahadi na majukumu yake wananchi waliomchagua wamuondoe kwa kura au utaratibu maalum utakao wekwa.Pia kwamaoni yangu;
- Sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma imulike maana haiwamuliki watumishi wenye ukwasi wa kutisha,pia haikagui hata taarifa za watumishi wa kawaida hilo lilithibitishwa bungeni kwenye awamu iliyopita na Mkosamali aliyekua mbunge wa Muhambwe kua hajawahi kukaguliwa