Rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kuzipunguzia kodi taasisi za kidini zinazotoa huduma kwa jamii

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Kwa Ufupi,
Leo Rais Magufuli ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika kanisa la kiaskofu, Jimbo kuu Katoliki Moshi na kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT).

Amewataka waumini na watanzania kuendeleza amani iliyopo nchini kwani ndio chachu ya maendeleo, amesema Urais wanao wao hivyo kuwaomba waendelee kumuweka katika sala zao ili kazi ya Urais ismpe kiburi.

Aidha Rais Magufuli ameahidi kuangalia uwezekano wa kuzipunguzia kodi taasisi za kidini zinazotoa huduma kwa jamii ikiwemo afya na elimu. Rais alikuwa akijibu ombi la askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT).

Zaidi, soma hapa chini..

Magufuli 1.jpg
Magufuli 2.jpg

Maguful.JPG
 
Na afanye kwa vitendo, aache kiburi na ujeuri dhidi ya mabosi wake hasa Jaji Lubuva aliyemchagua na kumpangisha magogoni. Awasikilize na achukuwe ushauri wa mabosi wake. Haiwezikani katika watanzania 50mil yeye pekee yake ndio mwenye akili kuliko 50mil.
Tushamchoka kumuombea ende akatuombee yeye sasa. Majumbani kwetu hakuna makanisa wala misikiti ya kuombea Viongozi wajeuri na viburi
 
hivi kura halali za urais bwana yule alipata kura ngapi?..."ninatangaza matokeo kama ninavyoyapokea kutoka kwenye vituo vya kupigia kura"
heh,bastola ya nini tena?(in tupa tupa writing)
 
Nini kimempata mkurugenzi wa mawasiliano ikulu Ndugu Msigwa?
Naona anawakilishwa na Haniu.
Kulikoni??????
 
Hakujua kama Kilimanjaro ni nchi nyingine kumbee..... Arudi tuu ugogoni kule akili zimeishia kwenye viwavivijeshi
 
Naona ameanza kujirudi, nazani ni kwasababu uchaguzi unakaribia karibia

Akili zao hawa viumbe wa CCM inajirudia pindi uchaguzi unapokaribia, wakishamaliza kuchaguliwana kwa magoli ya mikono wanakuwa wajeuri sana mpaka unatamali kuwazaba makofi. Hakuna aneyeniboa kama Lile likamanda Sirro liongo sana linapenda kuwafanya watanzania wajinga kwa uongo wake
 
Bavicha wamekasirishwa sana na ziara ya Rais wetu Kilimanjaro,walijipanga kumchafua kwa kebehi na matusi mitandaoni,ili wakazi wa kilimanjaro wamsusie Rais wao.
Ziara inaonekana imefanikiwa kwa 100%,bavicha wamebaki kutoa kauli za kibaguzi humu,wekeni akiba ya maneno jamani
 
Bavicha wamekasirishwa sana na ziara ya Rais wetu Kilimanjaro,walijipanga kumchafua kwa kebehi na matusi mitandaoni,ili wakazi wa kilimanjaro wamsusie Rais wao.
Ziara inaonekana imefanikiwa kwa 100%,bavicha wamebaki kutoa kauli za kibaguzi humu,wekeni akiba ya maneno jamani

Huu ushauri naona bora ungeenda kumpa Magufuli, aache jazba na ujeuri dhidi ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom