Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ametoa taarifa kuwa Wakuu wa nchi wa SADC wamekipitisha rasmi Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya SADC.
Rais Magufuli, ambaye hivi punde ametoa hotuba ya kufunga Mkutano huo huko Dar es Salaam, amesema kuwa kwakuwa kihistoria Kiswahili ni lugha ya Waafrika na ilitumika kutuunganisha hasa wakati wa kujikomboa, kupitishwa kwake ni kufuta machozi ya ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwenyekiti Magufuli amesema kuwa kiujumla, Mkutano huo wa 39 wa SADC, umekuwa wa mafanikio makubwa kutikana na yaliyojadiliwa na kuamuliwa na Wakuu wa Nchi wanachama. Amegusia kujiunga kwa Burundi kwenye SADC na kuhusu vikwazo vya Zimbabwe.
Kongole kwa viongozi wote wa Tanzania walioanzisha, kusimamia na kuwezesha kupitishwa kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya SADC. Najivunia Kiswahili, najivunia kuwa mtanzania!