Rais Magufuli: Kibamba mmejicheleweshea wenyewe maendeleo kwa kukosa mbunge sahihi huko nyuma ila sasa Mtemvu atawavusha!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,897
141,831
Rais Magufuli leo amewashukuru wananchi wa Kibamba kwa kumpa kura nyingi wakati wa uchaguzi mkuu na pia kuchagua mbunge na madiwani wote wa CCM.

Rais Magufuli amesema Kibamba wamejicheweshea wenyewe maendeleo kwa kushindwa kuchagua mbunge sahihi huko nyuma ambaye kwa muda wote amefanikisha kujenga km 5 tu za barabara ya lami.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa kufanya kosa siyo kosa ila kurudia kosa ndio tatizo hivyo amewapongeza wananchi hao kwa kumchagua Mtemvu wa CCM na amewaahidi ujenzi wa barabara zote jimboni humo.

Rais Magufuli amesema Mtemvu ni mnyenyekevu na kwa kuanzia amempa heka 52 za ardhi ili zitumiwe na wananchi wa kibamba kwa ujasiriamali na miradi yao mbalimbali.

J J Mnyika wa Chadema ndio mbunge mstaafu wa Kibamba

Source: TBC

Maendeleo hayana vyama!
 
Kongwa ingekua kama London kwani haiwajawahi kua na mbunge asie wa CCM miaka 60 ya uhuru lakini bado wanajisaidia vichakani, watoto wanakaa chini na kwenye vichaka. Hakuna madawati, hakuna madarasa watoto wanasomea vichakani.

Dodoma yote sasa hivi ingekua New York kwani hawajawahi kuchagua mbunge wa upinzani miaka 60 lakini zaidi ya nusu ya wakazi wa Dodoma ni omba omba.
 
Mbona hutaji jimbo la Mwanga!
 
Njombe yetu ingekua kama Stockholm kama hoja ingekua kua na wabunge wa CCM maana haijawahi kua na Mbunge wa upinzani tena kwa mkoa mzima.

Nadhani mheshimiwa ajikite kuiendeleza Tanzania bila kujali anafanya kazi na nani.Je fedha inayotumika sasa imeletwa na mbunge au miradi ilichelewesha kuwahujumu wabunge wa upinzani kwa gharama za wananchi?

Jibu nadhani ilikua na kucheza na maisha ya wananchi kujinufaisha kisiasa jambo ambalo ni kukosa uzalendo.afterall sijaona kilichochange maana kama ni mradi wa stend ni Progaram iliundwa kabla 2012 na kuanza utekelezaji 2013 kwa awamu na aliye chagiza ni world Bank.

Kama ni barabara huwezi tumia Morogoro road kupima uwezo wa mbunge. Atwambie labda mambo ya mitaani hapendi matatizo ya wananchi yafikie serikalini kupitia vya upinzani.
 
Kongwa ingekua kama London kwani haiwajawahi kua na mbunge asie wa CCM miaka 60 ya uhuru lakini bado wanajisaidia vichakani, watoto wanakaa chini na kwenye vichaka. Hakuna madawati, hakuna madarasa watoto wanasomea vichakani.

Dodoma yote sasa hivi ingekua New York kwani hawajawahi kuchagua mbunge wa upinzani miaka 60 lakini zaidi ya nusu ya wakazi wa Dodoma ni omba omba.
Hii comment itamfanya mleta uzi aukimbie uzi wake
 
Back
Top Bottom