Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Sikutaraji kuona Rais Magufuli akiwa na umahiri mkubwa wa kucheza na siasa za Tanzania kiasi hiki. Awali nilikuwa na hofu juu ya uwezo wake kwenye siasa za majukwaani. Ila kadri siku zinavyoenda, hakika anadhihiri kuwa ni mtu mwenye kiwangu cha juu sana katika siasa.
Hivi sasa wapinzani wanacheza muziki wa Rais Magufuli. Wapende wasipende lazima wacheze tu. iwe wamelala ama wamekaa. Iwe wamesimama ama wamechuchumaa. Lazima wacheze Muziki wa Rais Magufuli.
Kwa sasa imedhihiri kuwa kila Rais Magufuli anaposimama jukwaani na kuongea na Watanzania, viongozi wa upinzani wanatega masikio na kukodoa macho yao kodo ili kuona nini Rais anataka kuongea juu yao.
Siku zote Rais Magufuli amekuwa akiwafanya wapinzani wakose hoja na badala yake wanahangaika na matukio. Walianza na safari za nje. Wakaja na utumbuaji majipu. Na sasa wanahangaika na wanafunzi vilaza. Naamini kuanzia kesho, wapinzani wataitisha Press Conference ya kumtaka Rais afute kauli yake ya kuwaita wapinzani ni vilaza. Hili ni tukio ambalo tayari wapinzani wamelichukua na litaendelea kuwasumbua mpaka Rais atakapowatengenezea tukio jingine.
Kwa vile uwezo wao wa kufikiri ni mdogo na wengi wao ni vilaza na vihiyo, Rais Magufuli anawageuza atakavyo kama chapati jikoni. Bye bye Upinzani Tanzania