Rais Magufuli kathibitisha kuwa watendaji wengi wa Serikalini ni watu dhaifu, wenye elimu ndogo, magoigoi na wababaishaji

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,902
10,502
Huwa najitahidi kufuatilia ziara mbalimbali za Rais magufuli hasa zile za uulizaji wa maswali ya papo kwa papo kwa viongozi wa chini wanaohusika na miradi mbalimbali, nikabaini, watendaji wengi wa serikalini ni watu dhaifu, wenye elimu ndogo, magoigoi na wababaishaji.

Management by walking (MBWA) anayoifanya Rais magufuli inatuthibitishia ni kwa kiasi gani bila Rais Magufuli hakuna kinachoweza kwenda.

Mainjinia hawajui wanachokifanya, wakurugenzi wapo wapo tu hawajui hata takwimu za miradi, hawajui makadirio ya kazi, hawajui nani anapaswa kukamilisha kazi, hawajui kiasi cha fedha kilichotolewa....hawajui kitu. Wapo tu!

Maswali ya papo kwa papo anayowauliza Rais Magufuli yanaonesha hawana clue yoyote juu ya wanachokifanya.

Rais Magufuli ameonesha ni namna gani Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa ya watendaji.

Injinia gani huwezi kujieleza angalau sentensi mbili uueleze umma mpangilio wa mradi wote?

Ndio kusema kwamba, bila Rais Magufuli hamuwezi kufanya lolote?

Si ajabu miradi mingi inafanywa na wachina maana serikali imebaini hawa watanganyika ni lazy tu na incompetent.
 
Hivi kipimo cha utendaji wa kazi ni kuulizwa swali na kujibu?

Bado hatuamini kuwa mtu anaweza kushindwa mtihani akawa na maarifa ya kutosha tu ya kufanya mambo kuliko aliejibu maswali?
Nadhani kunae haja ya kujua tunataka wajibu maswali kwa ufasaha au tunataka watenda kazi?

Kwa Msingi wa hoja kama hiyo hata Joni hastahili maana kuna vipanga vinaongea kwa ufasaha na uwezo mkubwa kabisa wa kujieleza kuliko bwana Joni.

Ila bwana Joni tumemsokomezea na mambo yanaenda tu.
 
Huwa najitahidi kufuatilia ziara mbalimbali za Rais magufuli hasa zile za uulizaji wa maswali ya papo kwa papo kwa viongozi wa chini wanaohusika na miradi mbalimbali, nikabaini, watendaji wengi wa serikalini ni watu dhaifu, wenye elimu ndogo, magoigoi na wababaishaji.

Management by walking (MBWA) anayoifanya Rais magufuli inatuthibitishia ni kwa kiasi gani bila Rais Magufuli hakuna kinachoweza kwenda.

Mainjinia hawajui wanachokifanya, wakurugenzi wapo wapo tu hawajui hata takwimu za miradi, hawajui makadirio ya kazi, hawajui nani anapaswa kukamilisha kazi, hawajui kiasi cha fedha kilichotolewa....hawajui kitu. Wapo tu!

Maswali ya papo kwa papo anayowauliza Rais Magufuli yanaonesha hawana clue yoyote juu ya wanachokifanya.

Rais Magufuli ameonesha ni namna gani Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa ya watendaji.

Injinia gani huwezi kujieleza angalau sentensi mbili uueleze umma mpangilio wa mradi wote?

Injinia unababaika tu huelewi A wala B? Unafanya nini kazini?

Ndio kusema kwamba, bila Rais Magufuli hamuwezi kufanya lolote?

Si ajabu miradi mingi inafanywa na wachina maana serikali imebaini hawa watanganyika ni lazy tu na incompetent!

"Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?"

Pole sana Tanganyika!
Wakurugenzi na maDc ndo walipaswa wawasimamie hao wataalam, lakini wengi wao wapo pale kwa kuwa ni wakereketwa wa chama ,hawana Elimu, ni dhaifu mradi tu ajue kusema chama oyeee anapewa cheo.
Siku chama kikiacha kushika hatamu tutapata maendeleo
 
Hivi kipimo cha utendaji wa kazi ni kuulizwa swali na kujibu?

Bado hatuamini kuwa mtu anaweza kushindwa mtihani akawa na maarifa ya kutosha tu ya kufanya mambo kuliko aliejibu maswali?
Nadhani kunae haja ya kujua tunataka wajibu maswali kwa ufasaha au tunataka watenda kazi?

Kwa Msingi wa hoja kama hiyo hata Joni hastahili maana kuna vipanga vinaongea kwa ufasaha na uwezo mkubwa kabisa wa kujieleza kuliko bwana Joni.

Ila bwana Joni tumemsokomezea na mambo yanaenda tu.
nosense. hoja ni kuwa inakuwaje kiongozi hajui kinachoendelea kwenye eneo lake la kazi. hajui ni kiasi gani cha hela kimetengwa mfano kwa ajili ya barabara za wilaya
 
Tunawateua ki-sifa sifa, ndo maana tunawatengua kisifa sifa za kisiasa. Yaani kila kona siasa imeingia awamu hii, ndo maana tunazidi kushuhudia maigizo zaidi ya wale wa milingotini (KAOLE)
 
Kuijadili sana watendaji wa hii swerikali ni kupoteza tu mda...

Kwenye miradi kila mtu anakuja na mkandarasi wake na anataka kwenye tenda amwekee %
 
Hoja za mleta bandiko zina ukweli kwa namna fulani. Ni kweli ukiangalia watendaji wengi wanakosa kujiamini, na ubunifu. Wengi wanashindwa kuja na majibu ya haraka ya changamoto zilizopo. Hoja hii inafikirisha sana, Je, ni mfumo wetu wa kuandaa wataalamu wetu una shida au mfumo wa kuwapata watendaji wa Serikali yetu sio mzuri?

Kiukweli ukimuangalia Rais wetu ana nia njema lakini watendaji wake wengi (Sio wote) bado wana uwezo mdogo wa kutekeleza matamanio ya kiongozi wetu mkuu na matarajio wananchi walio wengi.

Naona kuna haja ya kufumua mfumo wetu wa elimu au mfumo wetu wa kuwapata wataalamu wetu baada ya kufanya uchambuzi na tafakuri ya kina juu ya kiini cha matatizo yetu.
 
Huwa najitahidi kufuatilia ziara mbalimbali za Rais magufuli hasa zile za uulizaji wa maswali ya papo kwa papo kwa viongozi wa chini wanaohusika na miradi mbalimbali, nikabaini, watendaji wengi wa serikalini ni watu dhaifu, wenye elimu ndogo, magoigoi na wababaishaji.

Management by walking (MBWA) anayoifanya Rais magufuli inatuthibitishia ni kwa kiasi gani bila Rais Magufuli hakuna kinachoweza kwenda.

Mainjinia hawajui wanachokifanya, wakurugenzi wapo wapo tu hawajui hata takwimu za miradi, hawajui makadirio ya kazi, hawajui nani anapaswa kukamilisha kazi, hawajui kiasi cha fedha kilichotolewa....hawajui kitu. Wapo tu!

Maswali ya papo kwa papo anayowauliza Rais Magufuli yanaonesha hawana clue yoyote juu ya wanachokifanya.

Rais Magufuli ameonesha ni namna gani Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa ya watendaji.

Injinia gani huwezi kujieleza angalau sentensi mbili uueleze umma mpangilio wa mradi wote?

Injinia unababaika tu huelewi A wala B? Unafanya nini kazini?

Ndio kusema kwamba, bila Rais Magufuli hamuwezi kufanya lolote?

Si ajabu miradi mingi inafanywa na wachina maana serikali imebaini hawa watanganyika ni lazy tu na incompetent!

"Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?"

Pole sana Tanganyika!
Siyo kwamba yeye ndie hajui cha kufanya wala helewi majukumu yake kweli?

Watumishi wengi kwa sasa hawafanyi kazi zao za kimuundo, wanafanya kazi kwa kutumwa na kuagizwa tu! Mara tekeleza hili mara lile! Mwisho wa siku anahikuta yuko bize kwa kazi za kutumwa na kikurupushwa tu.....akiulizwa majukumu yake ya msingi anakuwa hajafanya!

Mzee aache kuwatumikisha watumishi wa umma kama Ng'ombe! Ahakikishe kwanafanya kazi kwa mujibu wa miongozo, taratibu na sheria za kazi...
Ndio maanabnasema tatizo ni yeye kuyokujua wajibu wake!
 
Hapana uteuzi wao una kasoro kubwa. Huwezi ukamteua mtu ambaye HAKUKULIA kwenye Utumishi wa Umma na kuja kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi Mtendaji.
 
Huwa najitahidi kufuatilia ziara mbalimbali za Rais magufuli hasa zile za uulizaji wa maswali ya papo kwa papo kwa viongozi wa chini wanaohusika na miradi mbalimbali, nikabaini, watendaji wengi wa serikalini ni watu dhaifu, wenye elimu ndogo, magoigoi na wababaishaji.

Management by walking (MBWA) anayoifanya Rais magufuli inatuthibitishia ni kwa kiasi gani bila Rais Magufuli hakuna kinachoweza kwenda.

Mainjinia hawajui wanachokifanya, wakurugenzi wapo wapo tu hawajui hata takwimu za miradi, hawajui makadirio ya kazi, hawajui nani anapaswa kukamilisha kazi, hawajui kiasi cha fedha kilichotolewa....hawajui kitu. Wapo tu!

Maswali ya papo kwa papo anayowauliza Rais Magufuli yanaonesha hawana clue yoyote juu ya wanachokifanya.

Rais Magufuli ameonesha ni namna gani Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa ya watendaji.

Injinia gani huwezi kujieleza angalau sentensi mbili uueleze umma mpangilio wa mradi wote?

Injinia unababaika tu huelewi A wala B? Unafanya nini kazini?

Ndio kusema kwamba, bila Rais Magufuli hamuwezi kufanya lolote?

Si ajabu miradi mingi inafanywa na wachina maana serikali imebaini hawa watanganyika ni lazy tu na incompetent!

"Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?"

Pole sana Tanganyika!
HUONI JUZI WAMESEMA WENYEWE WAKO KWA AJILI YA NJAA AU TUMBO
 
Hoja za mleta bandiko zina ukweli kwa namna fulani. Ni kweli ukiangalia watendaji wengi wanakosa kujiamini, na ubunifu. Wengi wanashindwa kuja na majibu ya haraka ya changamoto zilizopo. Hoja hii inafikirisha sana, Je, ni mfumo wetu wa kuandaa wataalamu wetu una shida au mfumo wa kuwapata watendaji wa Serikali yetu sio mzuri?

Kiukweli ukimuangalia Rais wetu ana nia njema lakini watendaji wake wengi (Sio wote) bado wana uwezo mdogo wa kutekeleza matamanio ya kiongozi wetu mkuu na matarajio wananchi walio wengi.

Naona kuna haja ya kufumua mfumo wetu wa elimu au mfumo wetu wa kuwapata wataalamu wetu baada ya kufanya uchambuzi na tafakuri ya kina juu ya kiini cha matatizo yetu.

Mkuu uko sahihi, hebu sema elimu iweje ili tuone ubora, tofauti na tunachoona sasa?
 
Ukifanya kazi sekta binafsi kisha ukaenda Serikalini, aisee utajua Serikalini ni kula shushu tu na kupiga soga...

kwanza Serikalini hawajui kama kuna kitu kinatiwa Timesheet..... huwezi kula muda wa mwajili hata dk kumi, kabla muda wa msalani.
 
Back
Top Bottom