Rais Magufuli, karibu utumbue UDOM, kuna watumishi wanakwamisha malipo ya wanufaika wa mkopo kutoka HESLB

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Udom hasa COED watumishi wanakwamisha malipo ya wanufaika wa mikopo HESLB. Wakisaini wanasubiri hadi mwezi uishe ndipo pesa zao walipwe kwanini ichukue muda wote huo?

Wakiulizwa wanasema eti malipo yapo benki, wakienda benk wanaambiwa malipo hayajapelekwa. Yaani ni tabu tupu.
 
Wameziweka fixed deposit, au?
Serikali ichague viongozi imara na wasio na huruma vyuoni. Ofisi za uhasibu vyuoni ni aibu tupu. Walizoea kupiga pesa za wanafunzi hewa kwa ushirika na Bodi ya mikopo. Walizoea kupiga pesa za wanafunzi marehemu. Watu kama hao hawawezi hata siku moja kugeuka wakawa wema kwa ufuatiliaji wa Rais aliyeko Magogoni.
 
Huenda zipo fixed account kweli, yaani unaambiwa wanafunzi huko ni vilio tu, wanasaini ila hela kuipata ndo shughuli. Wengine wanaambiwa hela zao zilirudi bodi ila wakienda bodi wanaambiwa hazijarudishwa. Sasa haieleweki zipo wapi.
 
Hebu acheni kutoa vituhuma uchwara bila kufanya utafiti. Hivi unadhani ni rahisi kivile? Yaani uchukue pesa za wanufaika wote uweke fixed account kweli? Unajua zoezi hilo litahitaji kushirikisha watu wangapi? Na kwanini isiwe kwamba wamesaini kabla ya pesa kuja ili taarifa zipelekwe loan board kwanza ili wapate kujiridhisha juu ya wanufaika walipoko kabla ya kudiposit? Yaani nyie vijana ambao hamjakalia ofisi yoyote ya umma taabu kweli.
 
Hilo suala mbona linaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia serikali yenu ya wanafunzi na pia uongozi wa chuo! Likishindikana kabisa, Waziri mwenye dhamana(Profesa Ndalichako)bado anaweza kabisa akalipatia ufumbuzi unaohitajika.

Inashangaza awamu hii kila jambo anatakiwa rais alipatie ufumbuzi! Nadhani kuna utofauti mkubwa na awamu zilizopita. Wakati fulani Rais anatakiwa aachwe ili apambane na changamoto nyingine zinazolikabili Taifa.
 
Hebu acheni kutoa vituhuma uchwara bila kufanya utafiti. Hivi unadhani ni rahisi kivile? Yaani uchukue pesa za wanufaika wote uweke fixed account kweli? Unajua zoezi hilo litahitaji kushirikisha watu wangapi? Na kwanini isiwe kwamba wamesaini kabla ya pesa kuja ili taarifa zipelekwe loan board kwanza ili wapate kujiridhisha juu ya wanufaika walipoko kabla ya kudiposit? Yaani nyie vijana ambao hamjakalia ofisi yoyote ya umma taabu kweli.

Wanaposaini, hela zao zinakuwa tayari zimewekwa kwenye akaunti ya chuo.

Uhakika ni kwamba "sheet" za kusaini zinakuwa zimegongwa muhuri wa malipo (PAID)
 
Hebu acheni kutoa vituhuma uchwara bila kufanya utafiti. Hivi unadhani ni rahisi kivile? Yaani uchukue pesa za wanufaika wote uweke fixed account kweli? Unajua zoezi hilo litahitaji kushirikisha watu wangapi? Na kwanini isiwe kwamba wamesaini kabla ya pesa kuja ili taarifa zipelekwe loan board kwanza ili wapate kujiridhisha juu ya wanufaika walipoko kabla ya kudiposit? Yaani nyie vijana ambao hamjakalia ofisi yoyote ya umma taabu kweli.
Vijana wanadai kutoambiwa ukweli, huwezi kusaini hela hazijafika. Wamesema pande mbili zinawajibu sivyo. Nadhani kuna haja ya kuwasikiliza ktk hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana tunatawaliwa mpaka na Viongozi wapuuzi yaani utakuta mtoa Mada ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Yaani kazi kama ya kuangaika na watumishi wa UDOM Mkuu wa nchi ndo aje awawajibishe ? kwamba taarifa mmeshindwa kuwapa utawala wa chuo ?

Achaneni na upuuzi wenu ,wewe ndo unatakiwa kutumbuliwa .
 
Hebu acheni kutoa vituhuma uchwara bila kufanya utafiti. Hivi unadhani ni rahisi kivile? Yaani uchukue pesa za wanufaika wote uweke fixed account kweli? Unajua zoezi hilo litahitaji kushirikisha watu wangapi? Na kwanini isiwe kwamba wamesaini kabla ya pesa kuja ili taarifa zipelekwe loan board kwanza ili wapate kujiridhisha juu ya wanufaika walipoko kabla ya kudiposit? Yaani nyie vijana ambao hamjakalia ofisi yoyote ya umma taabu kweli.
Jiwe gizani nini!!.., mbona umeandika kwa uchungu hivyo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe gizani nini!!.., mbona umeandika kwa uchungu hivyo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Vijana mna hoja ya msingi kusaidiwa, tusijifanye hatujui tabia za management za vyuo pia ikumbukwe kua viongozi wengi wa taasisi za Umma ni "miungu wadogo" nina uhakika kuna tatizo mahali hapo chuoni kwao hivyo si vyema kubeza tatizo lao...wana hoja ya msingi ni vile hawajui nani wa kumfunga paka kengele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mbona ni mchezo wa siku nyingi sana hapo UDOM, pesa wanazi fix Bank then wanapata cha juu, lakini sio kila swala mpaka JPM aingilie si kuna waziri wa Elimu kwani halioni hili? UDOM pameoza tangu zamani, . Nakumbuka mwaka 2010 kuna wanafunzi wa kozi moja ya PPM wanafunzi wapatao 220 kila mmoja alitumiwa tzs 550,000 kwa ajili ya kwenda field lakini cha ajabu hizo pesa zikapigwa juu kwa juu wale wanafunzi hawakupewa hata senti wakaenda field kwa gharama zao, ila kwa sasa wanakatwa na bodi ya mikopo mpaka leo.
 
Ndo maana tunatawaliwa mpaka na Viongozi wapuuzi yaani utakuta mtoa Mada ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Yaani kazi kama ya kuangaika na watumishi wa UDOM Mkuu wa nchi ndo aje awawajibishe ? kwamba taarifa mmeshindwa kuwapa utawala wa chuo ?

Achaneni na upuuzi wenu ,wewe ndo unatakiwa kutumbuliwa .

Mkuu, mbona povu hivyo? Au wewe ni mhusika? Mada inajieleza kuwa wamefanya ufuatiliaji ngazi zote na majibu wanayopata ni hayo.

Kwa mfano, kama serikali ya wanafunzi wamefatilia lakini wakagonga mwamba, wahanga wakafatilia wakagonga mwamba, hapo unadhani kilio hicho kielekezwe wapi?
 
waziri ?.si mawizara si zipo Hapo UDOM ?
 
Udom hasa COED watumishi wanakwamisha malipo ya wanufaika wa mikopo HESLB. Wakisaini wanasubiri hadi mwezi uishe ndipo pesa zao walipwe kwanini ichukue muda wote huo?

Wakiulizwa wanasema eti malipo yapo benki, wakienda benk wanaambiwa malipo hayajapelekwa. Yaani ni tabu tupu.
Mchezo wa kuweka fixed deposit au watumishi kuzikopa fedha za mikopo ya wanafunzi ni kadhia kwa wanafunzi isiyostahili kuvumiliwa hata chembe. Watumishi wa aina hiyo isiwe rais tu ndio awatumbue. Inaelekea ni mtandao unaojinufaisha na fedha za mikopa ya wanafunzi na kuwaletea usumbufu mkubwa. Ni ufisadi unaostahili kutumbuliwa bila huruma.
 
Wachangiaji wengine humu ndo wapigaji, unakuta mtu anajifanya kujua kubwabwaja mara ooh, serikali ya wanafunzi, mara uongozi wa chuo mara sijui waz...We unadhani hao wanaolalamika ndo hawajui kama kuna ngazi zote hizo? wamehangaika kwenye ngazi zote hizo wakachoka tatizo halitatuliwi. Mi nimeshuhudia hadi watu wanasimamishwa masomo kisa wanafuatilia kesi kama hizo, mimi na kundi la wenzangu wengi tumewahi kwenda field tumeambia pesa zitatukuta huko hazikuja , someshwa mda zaidi tukiambiwa hela zinakuja hazikuja pesa ukijumlisha kama milioni kasoro efu 40, tumefika kwenye ngazi zote hizo ambako mchangiaji (anaejifanya anajua sana hadi kumuona mtoa mada mjinga ). Tuliwah hadi kutuma meseji kwa waheshimiwa sana watusaidie, piga simu hadi mwisho bila majibu, mtu unakaa chuo hujui utakula nini mchana na kesho ni test.....kwakweli akatumbue tu kama akipata mda!
 
Back
Top Bottom