Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,277
- 17,983
Tatizo ni sera za Serikali yenyewe. Angalia mfano wa mahindi. Walizuia kuyauza nje ya nchi. Matokeo yake bei imeshuka mno. Sasa wamefungulia lakini hakuna soko tena. Waganda sasa ndiyo wanauza kwenye masoko ya Tanzania.Mambo mengine ni kudhulumu watu tu. Kama Korosho zilinunuliwa kihalali kwa makubaliano kati ya Mnunuzi na Mkulima kosa ama tatizo liko wapi. Mbona wauza mahindi wengi siyo wenye mashamba ya mahindi.
Dhana ya biashara hapa iko wapi? Na wachuuzi iwe ni Kangomba ama wowote wale wanatokana na mfumo mbovu na mbaya wa masoko kwa mazao ya Kilimo nchini mwetu. Dunia nzima wauzaji wa mazao mara nyingi huwa si wakulima. La maana watozwe faini kwa kufanya biashara bila ya kuwa na leseni.
Ndiyo maana mkulima anaweza kuuza hayo maua apate chochote kuliko akose kabisa.
Serikali iwe mteja wa mahindi kama wengine.