Rais Magufuli: Kama una korosho na huna shamba hutalipwa

  • Hofu yangu ni kwamba mkishikilia korosho za mtu wakati alizinunua kwa makubaliano na mkulima, je itakuwa ni haki kweli?, maana mkulima ana haki ya kuuza korosho yake hata kwa shilingi mbili kwa kilo,maana ni mali yake
  • Hii practice ya Kangomba imeanza leo baada ya sakata la korosho au imekuwepo toka misimu iliyopita na je serikali ilifanya nini?
  • Kama mkulima anahitaji hela ya kwenda hospitali, kulipia ada ya mtoto akaweka bondi korosho zake then huyu aliyelipwa kwa korosho ana kosa gani?
  • Je ni kinyume cha sheria kumiliki korosho bila kuwa na shamba?
  • Je Kangomba ni kinyume cha sheria ya nchi, sheria gani hiyo?
  • Kama serikali haiwezi kuwalipa wenye korosho si iwaachie korosho zao wakaziuze wanapoona zinafaa, kwa nini serikali izishikilie?
  • Kama kangomba ni kinyume cha sheria ya nchi mbona hamjawakamata hao waliovunja hiyo sheria na kuwafikisha mahakamani?, na kama ni viongozi mbona hamjawapeleka kwenye tume ya maadili ya viongozi?
 
2020 ajiandae kuwa mwananchi wa kawaida kama sisi
Adobe_Post_20181202_225653.jpeg
 
Mambo mengine ni kudhulumu watu tu. Kama Korosho zilinunuliwa kihalali kwa makubaliano kati ya Mnunuzi na Mkulima kosa ama tatizo liko wapi. Mbona wauza mahindi wengi siyo wenye mashamba ya mahindi.

Dhana ya biashara hapa iko wapi? Na wachuuzi iwe ni Kangomba ama wowote wale wanatokana na mfumo mbovu na mbaya wa masoko kwa mazao ya Kilimo nchini mwetu. Dunia nzima wauzaji wa mazao mara nyingi huwa si wakulima. La maana watozwe faini kwa kufanya biashara bila ya kuwa na leseni.
 
Nimeambiwa kwamba wafanyabiashara wengine hutoa Korosho Msumbiji. Wakati wenzetu wakenya na waganda hawazuii mazao ya kilimo toka kwetu kuingia nchini mwao, sisi tunataka kuwafanya watanzania wanaoingiza Korosho toka Msumbiji ni wahalifu.

Serikali inunue zile korosho tu za wakulima, zile zingine za wasio na mashamba waache wenyewe wazitafutie masoko!
 
Hii practice ya uwepo wa mkulima then katikati kuna middle men, then baada ya middle men kuna wafanyabaishara wakubwa halafu baada ya hapo kuuzwa nje ambapo nako kuna minada ambayo wafanyabiashara husupply viwandani ndiyo chain ya biashara ya mazao ilivyo. Ukiingilia hiyo chain bila kujipanga unaharibu mfumo mzima wa mambo yanavyofanyika. HUWEZI KUMSAIDIA MKULIMA WA KOROSHO KWA KUMNING'INIZA MTEJA WAKE WA TOKA NITOKE, MAANA LEO UMEINTERVENE JE MSIMU UJAO NANI ATAKWENDA KUNUNUA HIZO KOROSHO KUTOKA KWA MKULIMA?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom