Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,469
- 1,697
- Thread starter
- #41
Nchi yetu ina karibia miaka 60 sasa, huo utajiri wa rasilimali tuko nao toka dunia imeumbwa, mbona hatuoni ukiakisi kwenye maisha ya wananchi waliowengi? Ina maana miaka yote 60 hatujajua njia nzuri ya kuutumia huo utajiri? Huu ni mwaka wa tano wa Magufuli madarakani, mbona huo utajiri bado haujaakisi zaidi ya deni la taifa kupaa kutokana na mikopo? Naomba iwekwe vizuri, nchi yetu ni tajiri au nchi yetu ina rasilimali nyingi? Maana naona hili neno utajiri linatumika kama Hadaa ya kiki ya kisiasa. Unapowaambia watu nchi ni tajiri lakini vijana hawana ajira, na wanaokubali nchi ni tajiri ni wale walio katika vyeo vya ulaji, ni kama kuwasanifu wananchi.
Sent using Jamii Forums mobile app