Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti Maandamano na migomo iliyokuwa fasheni ya huko tulikotoka

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wakati Rais Magufuli anatoa kauli hii, wapo waliobeza wakidhani kuwa haitekelezeki. Hata hivyo, hadi sasa ukweli ni kwamba Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti maandamano na migomo nchi nzima. Ukiona maandamano basi ujue ni ya kuunga mkono juhudi zake anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi. Hakuna mtutu wa bunduki wala virungu vilivyotumika kuzima migomo na maandamano. Ni mikwara yake tu pamoja na kushungulikia chanzo cha migomo na maandamano hayo.

Hongera Rais Magufuli. Kwa hili umeinyoosha nchi.
 
Tumeamua tu kuusoma mchezo ndiyo maana tupo kimya ila Kamanda Mkuu Mbowe akisema SU patawiva barabarani
Mnahuo uwezo Na makamanda wenu koko siku hizi!!! Hivi kweli Yule mzee ataongoza maandamano kama Slaa!! Ha aha ahaa

Sent from Moto G
 
Subiri tu hakuna muda utaanza kuona maandamano ya ugumu wa maisha, hiyo single ya kwamba anatetea wanyonge inaanza kuchuja kwa watu kuujua ukweli, walikuwa wanangoja nani alianzishe. Maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu, biashara zao zinazidi kuwa ngumu, wakulima ndio tunazidi kutekeketea. Halafu tunaambiwa mafisadi wanashughulikiwa, ukiuliza ni fisadi gani kufungwa, hakuna!! Watumishi na wafanyakazi hakuna aliyepandishwa mshahara kuendana na ugumu wa maisha. Halafu wananchi wanaishiwa kuonyeshwa maandamano ya wanaccm eti kumuunga mkono rais kwa utendaji wake!!
 
Wakati Rais Magufuli anatoa kauli hii, wapo waliobeza wakidhani kuwa haitekelezeki. Hata hivyo, hadi sasa ukweli ni kwamba Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti maandamano na migomo nchi nzima. Ukiona maandamano basi ujue ni ya kuunga mkono juhudi zake anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi. Hakuna mtutu wa bunduki wala virungu vilivyotumika kuzima migomo na maandamano. Ni mikwara yake tu pamoja na kushungulikia chanzo cha migomo na maandamano hayo.

Hongera Rais Magufuli. Kwa hili umeinyoosha nchi.

katika viwander alivofanikiwa hiki ndio kiwander kikubwa alichoweza kufanikiwa.
HONGERA MR. POMBE
 
Wakati Rais Magufuli anatoa kauli hii, wapo waliobeza wakidhani kuwa haitekelezeki. Hata hivyo, hadi sasa ukweli ni kwamba Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti maandamano na migomo nchi nzima. Ukiona maandamano basi ujue ni ya kuunga mkono juhudi zake anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi. Hakuna mtutu wa bunduki wala virungu vilivyotumika kuzima migomo na maandamano. Ni mikwara yake tu pamoja na kushungulikia chanzo cha migomo na maandamano hayo.

Hongera Rais Magufuli. Kwa hili umeinyoosha nchi.

HIVIII .. hata mie hapa mmenikamua kodi ya mjengo huu 15,000/=
muogopeni MOLA MAULANA!!
Hamuwezi kufanikiwa kwa kukusanya kodi za namna hii kama mmeshindwa kukusanya za MAKINIKIA
02.jpg
 
Wakati Rais Magufuli anatoa kauli hii, wapo waliobeza wakidhani kuwa haitekelezeki. Hata hivyo, hadi sasa ukweli ni kwamba Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti maandamano na migomo nchi nzima. Ukiona maandamano basi ujue ni ya kuunga mkono juhudi zake anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi. Hakuna mtutu wa bunduki wala virungu vilivyotumika kuzima migomo na maandamano. Ni mikwara yake tu pamoja na kushungulikia chanzo cha migomo na maandamano hayo.

Hongera Rais Magufuli. Kwa hili umeinyoosha nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu walikufa sana kwenye maandamano tena vijana, afadhari jpm umeokoa maisha ya watu
 
Na ndio maana wanasema ni dikteta uchwara,kwa sababu haongozi nchi kwa katiba bali udikteta kama huo.
 
Back
Top Bottom