Rais Magufuli jifunze kwa Rais Tayip Edorgan wa Uturuki

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,842
Rais wa Uturuki Bwana Tayip Edorgan aliomba mitandao ya kijamii nchini mwake ifungwe kabisa kwa sababu ilikuwa inaichafua serikali yake na yeye mwenyewe, Baada ya Muda mfupi, Jeshi lilifanya jaribio la mapinduzi, akiwa kwenye mapumziko kwenye mji mwingine hapo hapo UTURUKI, Muda mfupi baada ya kujulishwa kuwa Kikosi cha Jeshi kinataka kumpindua, Rais huyo haraka sana, aliondoka ndani ya Hotel aliyokuwemo, lakini wakati huo huo, akaukumbuka mtandao wa kijamii wa Whatsapp na Tweeter, Rais alijirecord akizungumza kwa sauti, akiwasihi wafuasi na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi mitaani kupinga jaribio hilo la kijeshi, Rais Edorgan aliutuma ujumbe huo na mara moja ukaanza kusambaa kwa kasi ya ajabu kwa wananchi, wananchi wa UTURUKI walipoona na kusikia sauti yake, walianza kumiminika mitaani wakiwapinga wanajeshi walioongoza mapinduzi hayo huku wanajeshi wengine wakipigwa na Raia waliojitokeza mitaani.

Hivyo, Rais Magufuli, tukio la uturuki linaweza kutoa somo Fulani kwako, ingawa si kwa dhana hiyo hiyo ya mapinduzi ya kijeshi la hasha, kunaweza kutokea tukio lolote ambalo serikali ingependa wananchi wote kwa haraka sana wapate taarifa au serikali yako inaweza kuwa na jambo Fulani ambalo ungependa upate mwitikio wa wananchi, hivyo, si busara sana kuanza kupambana na vyombo vya habari au mitandao ya kijamii, maana nyote mnahitajiana, Wewe unauhitaji mtandao wa Jamii forums na mtandao wa Jamii forums unakuhitaji, Mh, Rais kabla hujawa Rais mtandao huu ulikuwepo, na wenzio wote waliuacha, sasa kwa nini wewe tu ndo uumie?

Serikali ina siri gani ambayo hamtaki iandikwe humu? hivi kama kuna Jaribio la mapinduzi ya kijeshi limepangwa dhidi yako, na mtandao huu ukaliibua, hivyo kuzimwa haraka, huwezi kushukuru huu mtandao? au kama Tanzania imevamiwa unataka tusihabarishwe? au kama kuna wizi umetokea sehemu Fulani na ukaandikwa humu ina maana napo ni dhambi?

Tafakari sana Mh. Rais, tulianza kuwa na Imani na wewe, ila kwa jinsi unavyoenda, inatia shaka sana, kibaya Zaidi, huu ni mwaka wa kwanza tu toka umeingia madarakani, tunajiuliza, je ikifika miaka 5 hali itakuwaje?
 
Watawala wa ki imla siku zote huogopa mawazo mbadala
Tumshauri ili apate mapumziko ya moyo afanye kama China aanzishe mtandao wake wa serikali na aifungie mingine yote mpaka atakakapoondoka (kama ataondoka)
 
Hongera kwanza...
Pili..Pomb@ hana akili hiyo na hataki kushauriwa yeye anawaza ndege tu na siyo kingine ....
Kama nilivyosema akili yake anaifahamu MKEWE ukiona imefikia muda MWALIMU anamkimbia mumewe tena wazir ...fahamu kuna Shida sana...
 
unajua niliwahi kufikiria kuhusu uwazi na demokrasia JK aliaachia. Niligundua huyu mtu aliona mbali.
unapokandamiza watu,hawana sehemu ya kupumua then ndio unasababisha tukio. Wacha watu waseme wanalotaka kusema with both positive and negative criticism lakni at the end of the day unajua umesimamia wapi.
kingine ukusanyaji wa habari ni rahisi sana maana watu watasema kla jambo mtandaoni. mimi naona ni bora kuacha social media zisiingiliwe ili serikali ipate habari na kujifunza jambo
 
Back
Top Bottom