Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
Ishu ya Zanzibar imekaa kimtego sana kwa Rais Magufuli.
Anahitaji kuisolve kwa hekima sana, na katika kuisolve inapaswa asiwasikilize kabisa wale wenye mihemko ya kisiasa kutoka katika chama chake wanaowaza matumbo yao.
1. Zanzibar yenye machafuko haitomuacha salama
Jamii ya kimataifa inafuatilia kwa makini sana yanayotendeka nchini hususan Zanzibar.
Ni dhahiri Jumuia ya Kimataifa itakuwa tough tena tough sana kwa rais Magufuli iwapo rafu za kisiasa zitafanyika huko Zanzibar.
Na iwapo itatokea vifo vya kisiasa, Magufuli na wasaidizi wake na wahafidhina huko Zanzibar watakuwa katika hali ngumu sana na ninahofia wanaweza kufikishwa ICC. Kwa hiyo namshauri awe makini sana asikubali michezo michafu ya kutaka kuwaengua wagombea wenye ushawishi huko Zanzibar
2. Zanzibar isiyo na maridhiano ni mzigo mzito wa kiuchumi
Uchaguzi wenye magumashi huko Zanzibar utapelekea wahisani kutunyima mikopo nafuu, misaada na hata kufikia hali ya kuiwekea serikali ya JMT na ya Zanzibar itakayopatikana kibabe vikwazo vya kiuchumi.
hali hiyo italazimisha Rais wa Muungano kutumia resources zake kuibeba kifedha serikali ya SMZ iliyohohehahe, katika mazingira hayo rais atajikuta ana mzigo mzito wa kubeba serikali nzima ya SMZ na wakati huohuo nchi nzima ikiwa imefulia kutokana na vikwazo na kukosa mikopo.
Hali hiyo itapelekea JPM kama akiendekea na uraisi kujikuta anakosa pesa za kutekeleza miradi aliyoikusudia na pia kushibdwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi, Hii itasababisha wananchi wazidi kumchukia, na kukichukia chama chake na inaweza kupelekea hali ya maisha ya wananchi kuzidi kuwa mbaya zaidi ya iivyo sasa
3. Kuharibu uchaguzi Zanzibar kutakomaza mbegu ya kuvunja muungano
Wazanzibari walishaonyesha kutaka serikali tatu, na hili halitaondoka kwa kuondoka Maalim Seif katika ulingo wa kisiasa. Na Laiti vichwa makini nsani ya CCM vingeumiza vichwa vyao tena vingegundua kuwa wale wahafidhina huko Zanzibar ambao wanajifanya wafia chama ni kwa sababu ya madaraka tu waliyonayo,
Nje ya madaraka hao wote wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili. Kitendo cha kuvuruga uchaguzi na kucheza tena faulo kuwanyima Wazanzibar haki ya kumchagua wamtakaye kitaongeza chuki mioyoni mwao dhidi ya huu muungano, na hatimaye huu muungano itafikia hatua utakosa watetezi wengi kutoka upande wa Zanzibar, na ikifika hatua hatua hiyo hakuna jeshi wala nguvu itakayolazimisha huo muungano uwepo.
Ni haki peke yake kwa wananchi itakayolinda na kudumisha muungano, la sivyo huu muswada wa sheria wa kuwadhibiti akina maalim kugombea iwapo utapita na watawala wakalazimisha sheria ifanye kazi kwa kurudi nyuma basi itaaccelerate kufa kwa huu muungano huko mbeleni.
Ushauri wangu
1. Namshauri Rais Magufuli ajijengee legacy ya kukumbukwa kwa kuwatendea haki Wazanzibari, awape haki yao ya kuchagua wamtakaye bila figisufigisu
2. Iwapo Zanzibar itaangukia kwenye machafuko kwa sababu za kibabe mfano wa zile za mwaka 2015, safari hii international. community haitomuacha mtu salama, kuna watu watapekekwa ICC, namshauri asije kujikuta matatani baada ya yeye kutoka madarakani, ni bora kuchukua tahadhari mapema kwa kutenda haki.
3. Iwapo serikali ya CCM itamess up na ishu ya Zanzibar, basi ijiandae kubeba zigo zito sana la serikali hizi mbili kwa kutumia kodi za makabwela wa Tanganyika maana wahisani watakaza watakaza vyuma mno. Hii itapelekea JPM kushindwa kutimiza malengo yake ya miradi mbalimbali anayowaza kuifanya
Ni heri CCM na serikali yake ya sasa wakayatafakari haya la sivyo wanaweza kupata tabu sana hapo baadae!