My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Pamoja na kwamba ninaishi Australia, lakini wewe bado ni Rais wangu tu ,nipo hapa Australia kimwili tu, lakini kiroho nipo Tanzania.
Rais wangu, hata wewe huwa unasema kwamba "msema kweli ni mpenzi wa Mungu ".
Basi acha na mimi niseme kweli sasa ,Rais wangu Magufuli umezungukwa na kundi la watu wa ajabu kupindukia.
Urais ni taasisi, wewe Kama mkuu wa nchi umezungukwa na watu wa Kila aina, lakini kwanini yote haya yanatokea?
Wataalamu wa uchumi wapo tu wanaangalia? Wataalamu wa siasa na Diplomasia za kimataifa nao wapo tu wanaangalia?
Au pengine tatizo ni wewe labda hushauriki na sasa wameamua ni bora wakae kimya siku ziende.
Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nijikite tu na uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao wananchi wengi wameonekana kuususia na baada ya hapo wewe umeamua kuwabebesha msalaba wakuu wa mikoa kwamba kwanini watu hawajiandikishi ili kupiga kura.
Rais wangu, unataka wakuu wa mikoa wafanye nini juu ya hili? kwamba wananchi wakamatwe kisha wakajiandikishe na kupiga kura?..
Au wakuu wa mikoa waitishe mikutano kuwasihi na kuwabembeleza wananchi ili wajitokeze kupiga kura?
Wakuu wa mikoa wafanye nini ktk hili?
Umesema kwamba utawawajibisha endapo ktk mikoa yao wananchi hawatakuwa na mwitikio.
Hapa ndipo nimelazimika kukueleza Rais wangu uikimbie hasira ya Mungu.
Bahati mbaya zaidi, taifa la Tanzania halina watumishi shupavu wa Mungu, wanaoweza kusimamia kweli ya Mungu, nao wameingia Kwenye kundi la kusifia tu, hapana kukosoa.
Rais wangu, wewe ndo chanzo cha wananchi kukosa ari ya kushiriki uchaguzi, kauli zako huwa zinaegemea upande wa CCM tu na ni kauli za kibaguzi kabisa.
Hizi ni baadhi ya kauli zako za kibaguzi...
1."Ninakulipa mshahara, nimekupa gari halafu unatangaza mpinzani kashinda ".
2."Ole wake yoyote atakayempiga mtu aliyevaa kijani(CCM)
(Hapa ulipaswa kusema, Ole wake yoyote atakayempiga mtanzania)
3.CCM itatawala milele (Hakuna atawalaye milele zaidi ya Mungu)
Kwa kauli Kama hizo ,watu wameona kuwa wanapoteza muda bure kwa sababu washindi wanajulikana .
Rais wangu, ktk hilo wakuu wa mikoa watafanyeje ?.
Tenda haki ili uweze kujitenga na ghadhabu Mungu.