Rais Magufuli, ikimbie hasira ya Mungu

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Pamoja na kwamba ninaishi Australia, lakini wewe bado ni Rais wangu tu ,nipo hapa Australia kimwili tu, lakini kiroho nipo Tanzania.
Rais wangu, hata wewe huwa unasema kwamba "msema kweli ni mpenzi wa Mungu ".
Basi acha na mimi niseme kweli sasa ,Rais wangu Magufuli umezungukwa na kundi la watu wa ajabu kupindukia.
Urais ni taasisi, wewe Kama mkuu wa nchi umezungukwa na watu wa Kila aina, lakini kwanini yote haya yanatokea?
Wataalamu wa uchumi wapo tu wanaangalia? Wataalamu wa siasa na Diplomasia za kimataifa nao wapo tu wanaangalia?
Au pengine tatizo ni wewe labda hushauriki na sasa wameamua ni bora wakae kimya siku ziende.
Nina mengi ya kukueleza ila kwa leo nijikite tu na uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao wananchi wengi wameonekana kuususia na baada ya hapo wewe umeamua kuwabebesha msalaba wakuu wa mikoa kwamba kwanini watu hawajiandikishi ili kupiga kura.
Rais wangu, unataka wakuu wa mikoa wafanye nini juu ya hili? kwamba wananchi wakamatwe kisha wakajiandikishe na kupiga kura?..
Au wakuu wa mikoa waitishe mikutano kuwasihi na kuwabembeleza wananchi ili wajitokeze kupiga kura?
Wakuu wa mikoa wafanye nini ktk hili?
Umesema kwamba utawawajibisha endapo ktk mikoa yao wananchi hawatakuwa na mwitikio.
Hapa ndipo nimelazimika kukueleza Rais wangu uikimbie hasira ya Mungu.
Bahati mbaya zaidi, taifa la Tanzania halina watumishi shupavu wa Mungu, wanaoweza kusimamia kweli ya Mungu, nao wameingia Kwenye kundi la kusifia tu, hapana kukosoa.
Rais wangu, wewe ndo chanzo cha wananchi kukosa ari ya kushiriki uchaguzi, kauli zako huwa zinaegemea upande wa CCM tu na ni kauli za kibaguzi kabisa.
Hizi ni baadhi ya kauli zako za kibaguzi...
1."Ninakulipa mshahara, nimekupa gari halafu unatangaza mpinzani kashinda ".
2."Ole wake yoyote atakayempiga mtu aliyevaa kijani(CCM)
(Hapa ulipaswa kusema, Ole wake yoyote atakayempiga mtanzania)
3.CCM itatawala milele (Hakuna atawalaye milele zaidi ya Mungu)
Kwa kauli Kama hizo ,watu wameona kuwa wanapoteza muda bure kwa sababu washindi wanajulikana .
Rais wangu, ktk hilo wakuu wa mikoa watafanyeje ?.
Tenda haki ili uweze kujitenga na ghadhabu Mungu.
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
 
Una sababu gani kumchagua mtu ambaye kesho anauawa, anatekwa , anapotea. Hapana. Big No. Waache watawale milele.
 
msemaji uongo kwa jina la msemaji ukweli. wakala wa msema ukweli ni mpenzi wa Mungu wakati ni msema uongo. llogic imekukimbia. logic na uongo havichangamani hadi mwisho!
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
Andiko lako ni aibu kwako binafsi na kwa ccm pia , una macho yanayoona karibu mno !
 
Kumbe Siku hizi Tandale kumegeuka kuwa ni Australia? Basi na Mimi GENTAMYCINE japo nipo Washington Marekani Kimwili, ila Kiroho kabisa nipo Nyumbani Tanzania.
 
Hali si hali uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Nipo countryside huku watu hawana mwamko, mabalozi wa nyumba kumi (CCM) wenyeviti wa vitongoji na wenyeviti wa vijiji wanapita kuhamasisha ila watu hawataki, kuna bibi ni CCM damu damu ila amesikika akisema, namnukuu "nani aende kupoteza muda wake, viongozi tunaowataka mnawakatalia mbali kwa kuwaibia kura au kuwapoteza"

Shime tujitokeze kujiandikisha, maana tusipojiandikisha twajikomoa wenyewe, hatumkomoi yeyote yule.

Kupiga kura ni muhimu na kunampa mtu haki ya kuamua kuchagua mtu sahihi hata kama hatochaguliwa
 
Hizi porojo tu
We baki kwa mabeberu Siku ukirudi uanzie kushangaa terminal three Mambo yalivyopendeza
Ushamba mzigo hiyo terminal 3iliyojengwa tangu awamu ya nne mmembebesha Mungu wenu Magu? Mvua ndogo ya juzi maji yali jaa ndani ya jengo usipime. Labda hicho ndiyo atakuja kushangaa kuona Airport ya kimataifa mvua ikinyesha abiria mnatafutana si jambo la kawaida kwa vijana vya ndege
 
Hiyo takataka inayovuja ndio ya kushangaa ?? Ushawahi kutoka nje wewe takataka??
Labda ushangae kuvuja wewe umeona wapi kiwanja cha ndege cha kimataifa maji yana jaa? Ndiyo cha kushangaa
 
Hata nikitoka lazima niwe na return ticket
Siwezi kuishi kwa mabeberu Mimi

Kule ni kuzuri kwa mazingira ya nje tu lkn maisha ya kishetani mno
Watu wanatekwa na kuuwawa hovyo kama bongo? Au hiko nje wako wasiojulikana wanateka ma kuua ?
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa wizara ambayo inashughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iko kwenye ofisi ya Rais. Kwa maana nyingine, Boss wa Serikali za Mitaa ni Rais.

Pili, Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iko mikononi mwa Ofisi ya Rais.

Rais alichofanya ni kutimiza majukumu ya Ofisi kama ambavyo kanuni za utumishi zinavyomtaka.

Kwa upande wa kisiasa, Rais Magufuli na CCM hawana hasara yoyote kama watu wengi hawatajitokeza kwenda kupiga kura kwa sababu haiwaathiri katika majukumu yao ya kitaifa kwa sababu tatizo la political legitimacy lipo tokea mwaka 1995.

Kutojitokeza watu wengi kwenda kujiandikisha ni pigo kwa upinzani ambao unategemea nguvu ya madaraka kupitia sanduku la kura!

Haina mjadala kuwa watawala wa nchi za kiafrika huhofia sana wanapoona wananchi wengi wanakuwa na mwamko wa kutaka kupiga kura kwa sababu hii inayonyesha wanataka mabadiliko.

Jaribu kuangalia utagundua kuwa CCM walipata msukosuko katika chaguzi mbali mbali kutokana na wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.

Nihitimishe kwa kusema, Watu wengi kutojitokeza kwenda kujiandikisha ni sherehe kwa serikali iliyoko madarakani (CCM) na kilio kwa wale wanataka kuingia madarakani (Wapinzani).
Ndio maana tumesema, jitangazeni mmeshinda nchi nzima.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom