Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mzee Mkapa na Mzee Kikwete walikuwa na utaratibu wa kulihutubia taifa kila mwisho wa mwezi. Walitumia fursa hiyo katika kuelezea dira zao kikazi. Ulikuwa ni utaratibu uliowaweka karibu na wananchi ingawa upungufu wa utendaji wa awamu zao haukuweza kupungua kutokana na wao kuamua kujenga mahusiano ya karibu na wananchi kupitia hotuba zao.
Rais wa awamu ya tano haonekani kupenda kufuata tamaduni za wale waliomtangulia. Anapopata fursa ya kuhutubia katika shughuli fulani ya kiserikali, anahakikisha anaongea kwa uhuru mkubwa ili mawazo na maoni yake yaweze kuufikia umma. Rais huyu sio mwanasiasa, haongozi kwa nia ya kumfurahisha mtu au kundi fulani la watu, anasimamia katika kile anachokiamini. Yale makundi ya kijamii yaliyokuwa yakipata umaarufu kupitia ukosoaji wa hotuba za Mzee Mkapa na Mzee Kikwete, katika awamu hii watapoteza umaarufu wao.
Rais kaenda Ikulu kufanya kazi yenye faida kwa wote, anao udhaifu mwingi lakini ile sincerity yake ni neema kwa Tanzania.