Rais Magufuli hula chakula kilichopikwa na mkewe tu

Mkuu nisaidie sijapata mwanga




Hakuna mwanga wowote unaoweza kuupata toka kwenye thread hii ya mwendokasi,ni thread ya kipumbavu isiyo na maana yoyote na inayothibitisha uwezo wa watu wa kutunza kumbukumbu.Hivi kile chakula alichokula mgahawani pale Mwanza nacho alikipika mkewe?
 
Picha haionekami vizuri bado naendelea kusoma michango ya wadau wengine. Ila mlinzi wa kweli ni Mungu tu. Wengine maandiko yanatuambia hata tukinywa sumu, tukikanyaka nyoka hatutadhurika. Sijasoma hili gazeti, wamepata wapi hizi taarifa kuhusu mlo wa Rais?
 
Baada ya kutambuliwa kama mtu mwenye msimamo mkali na asiyependa dhihaka, ambaye huwafuta watu hadharani, huenda sasa Rais wa Tanzania John Magufuli ana maadui wengi.

Sasa akiwa ikulu na kama njia ya kuchukua tahadhari, inaripotiwa kuwa Magufuli hula chakula kilichopikwa tu na mke wake.
Kulingana na gazeti la Financial Times ni kwamba hili limedhihirika kutoka na upinzani anaokumbana nao. Lakini hilo halijathibitishwa wala gazeti la Financial Times halijasema ni jinsi gani walipata uvumi huo.


Chanzo: BBC Swahili
Acheni propaganda,,,,mxiuuuu!!
 
Sasa sisi inatuhusu nini? kwa hiyo hata siku ile alipokuwa kwenye mapumziko kule geita alipokula pale hotelini kile chakula alipikiwa na mke wake pale?
 
Huyu mkewe aliyekataa kumfanyia kampeni kutokana na kudhalilishwa hadi alipoombwa kufanya hivyo na watu mbali mbali ndani ya CCM akiwemo Maria Nyerere?
 
Haya ni mambo madogomadogo mno, naona hiyo BBC wamekosa la kusema, by the way kila nafsi itaonja umauti ni siku tu haijulikani na linapokuja suala kifo hata mkeo unayemuamini anaweza akakuua.
Sualala kupikiwa na mke hiyo ni privacy ya kwake kama binadamu ana uhuru wa kuchagua kuna wengine vyakula vya wake zao hawali.
 
Kwa hyo tusimuombee tena!!?mtu mwenyewe muoga kila siku anatusumbua tumuombee lakin anaogopa usalama wake hana imani huyu,,simuombei tena
 
Nangoja waje wakujibu hili swali . Im sure hawana majibu watatoa mimacho tu
Walichukua chakula chao kutoka nyumbani (ikulu) na kuviweka katika vibakuli zenye mifuniko.

Magu alirudisha wale wapishi wa Mkwere sehemu zao za awali na alisema siku hiyo mke wake ndio atatayarisha chakula chake.

Link Magufuli aifumua Ikulu
 
Kila kiongozi huwa na personal chef wake. Na hii hutokana na sababu nyingi moja wapo ikiwemo "taste". Kama Dr. President kaamua kuwa the first lady's recipes are the tastiest, its good for him!
 
Back
Top Bottom