Rais Magufuli hula chakula kilichopikwa na mkewe tu

Haya bhana. Kwa Mkwere kabla ya kula ilibidi wazee wa mlingotini waseme. Sasa ni lazima mkewe aseme. Ushirikina lakini kwa ni ikulu tunasema ni ushirikiano.
 
Habari zingine ni kutafuta Kiki tu, nani sasa anapikiwa chakula na hawara zaidi ya Padre Wilbroad Slaa??

Lakini kuna siku alikula Chakula mama Ntilie pale Airport Mwanza, sasa sijui kama Mama yetu Janet aliwahi pale asubuhi kupika ugali na kamongo
 
Ni uoga tu!
Hata maamuzi yake mengine yanajengwa juu ya hofu!
Kwani njia ya kumdhuru mtu ni kupitia chakula peke yake?
Na maji?
Na hewa?
Kushikana mikono?
Je analindwa na mkewe?
Anaendeshwa na nani kwenye gari?
Usafi wa ofisi unafanywa na nani?
N.k
halafu mtu asiyeamini watu wengine na kuonyesha waziwazi yeye ataaminiwaje?
Je hii mbinu ya kupikiwa na mke wake ni sustainable kwa muda wote wa uongozi wake?
 
Ni mkewe Huyo Atapika Ndio... Ila Atambue Kuwa Anaudhaifu kama Binadamu anaweza Lubuniwa One Day.. Na Watu wanaweza Pitia Huyo huyo Mkewe
 
Edward Hosea alikuwa hali chakula chochote ambacho hajaenda yeye mwenyewe kununua Sokoni.mf Nyama lazima anunue Mwenyewe hata akinunua Dereva wake hali.
Hii tabia sio nzuri. Itafika wakati hata huyo ngombe atafuga mwenyewe, nyanya, na vitunguu atalima mwenyewe. Kwa ujumla lazima tujenge tabia ya kuaminiana, isije ikafika mahali hata ukialikwa huli chakula kwa hofu ya kuuawa. Hatujafika huko ila kuna watu wanalazimisha tufike huko!
 
Misosi ya kustukiza huwa haina madhara.

Changamoto inaweza tokea iwapo mama atakuwa Ruvuma na mkuu yupo Mwanza, I mean wakiwa ziara toauti.
Hii taarifa yawezekana haina uhalisia. Hivi wakati ule alipokuwa Waziri wa Ujenzi mkewe alikuwa anaacha kufundisha anakwenda mpikia mumewe awapo Bungeni au ziarani? Hizi taarifa zinaweza kuleta hisia za kuanza kuwindana.
 
Mwanzoni nilipo iona hii siredi ni kajiuliza ujumbe gani uko hapa?

Kidogo kidogo picha inajileta kuna watu.
 
Sijaelewa lengo la hii habari! Sikuona logic ya Mambo mengi! Nadhani walitakiwa kusema huwa anapenda kula chakula alichopika mkewe! Njia za kumdhuru mbaya wako ziko nyingi Mno sasa kwanini chakula? Kwani ni njia moja ipo kwa ajili ya kumdhuru mtu? Yaani wote duniani waliowahi kudhuriwa wabaya wao walifanya kupitia chakula? Nilikuwa najaribu kupitia kumbukumbu zangu zikaniambia J. F. Kennedy , Samora Machel, Patrice Lumumba, Kabila Sr na Thomas Sankara wala wabaya wao hawakujua habari za chakula. Kiki nyingine zinaweza kuligawa taifa.
 
Back
Top Bottom