Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

suala la mifuko ya plastic na viroba ndio moja ya mambo ambayo sitayasahau awamu hii.
yamefanikiwa 100% hadi mtaani wanashangaa
 
Magufuli anataka kusema ucheleweshwaji wa azimio la kupiga marufuku mifuko ya plastic kwa more than 4 years ni kosa la January Makamba peke yake? Hizi lawama za kindezi sana. Yeye kama Rais alifanyaje kusort out the mess?
 
Bora akae kimya na wewe ukae kimya kwa sababu tutagombana, lini ulimuona au kumsikia makamba analaani manyanyaso zidi ya upinzani, kupigwa risasi, kufutwa ubunge, kuuawa wapinzani n.k. sasa yeye Zitto anajifanya kimbelembele kuwatetea maccm
OK OK ok, nanyamaza ili tusigombane. Ila nitafafanua baadae maana ya kiss the enemy of your enemy.
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini

Kuna sababu kubwa moja tu ambayo wewe hujaitambua ilomfukuzisha kazi January Makamba.

Rudi tena muongee kwa uzuri na atakwambia ni sababu ipi hiyo.

Au pia waweza kuwa unaitambua sababu hiyo lakini unazuga tu kwa kutafuta umaarufu.

Vinginevyo acha kusumbua akili za watu humu JF na wasomaji wetu.

Kumbuka, hapa JF ni kisima cha maarifa.
 
Nmeanza kumuelewa Pascal Mayala binafsi sio shabiki wa Mh Magufuli na Sera zake lkn khs Mjivuni Mh January na mjivuni Mh Nape nasimama na Mh Rais Ndugu Zitto Ruksa Kutetea wapigaji wenzio mnajifanya watetezi wetu ila Baada kunyimwa nafasi ya kuiba zaidi kwani ww mwenyewe unafikiri tumesahau kauli zako Rais Alipotembelea Kigoma na Bado mwaka 2020 muendeleze Biashara zenu au karibu tubebe box uku Safi sna Mh Magu...
 
Ndege wafananao huruka pamoja....bilashaka kuna madoadoa yameongezeka kwenye mabawa.
 
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa
Kasema kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ta fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha
Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagima kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
Itakuwa alikuwa anaangalia tu redio kama sio tv huku masikio kayaziba
 
Zitto alimtegemea sana January......muda si mrefu tutayasikia ya NSSF!
Unaweza kua na point but kwa muktadha hu hebu jibu HOJA za Zitto na mhe badala ya hayo mambo ya NSSF ambayo wengi tunayajua, kwenye NSSF wapo na sio Zitto peke yake, kwa ufupi usihamishe maada, tujadiri iliopo hewani kwanza
 
Magufuli anataka kusema ucheleweshwaji wa azimio la kupiga marufuku mifuko ya plastic kwa more than 4 years ni kosa la January Makamba peke yake? Hizi lawama za kindezi sana. Yeye kama Rais alifanyaje kusort out the mess?
 
We zitto unakuwaga taahira saa zingine, hivi hii hoja ya trillion 1.5 kuna wapuuzi wanaowaamini

Kwa mwezi tu TRA inakusanya wastani wa trillion 1.3 na katika matumizi almost billion 600 zinaenda kulipa mishahara, sasa eti mtu aibe trillion 1.5? Nchi ingesimana. Na itapelekwa wapi mipesa mingi hivyo? Acacia tu imenunuliwa na Barrick kwa billion 980 (japo ni uongo)
 
Back
Top Bottom