Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
751
3,086
JPM1.jpg

Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Arnold M. Kihaule kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa Vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na ofisi moja pekee ya NIDA.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo pamoja na kuzungumzia masuala mengine mbalimbali wakati akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma.

Kuhusu usajili wa NIDA, Rais amesema:

"Mkurugenzi ondoka sasa hivi Dar es Salaam uje hapa Morogoro kushughulikia hili tatizo la NIDA, Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA aje ashughulikie changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya ‘Guest’,na hili litazamwe nchi nzima watu wapewe vitambulisho”

''Leo uje hapa ukae na mkuu wa mkoa na wilaya muangalie namna ya kuseti namna ya kutoa huduma hizi kwa wananchi hawa. Na hili liwe pia kwa Tanzania nzima. Inawezekana matatizo haya hayapo hapa Morogoro tu''

''Hatuwezi kucheleweshwa na watu fulani fulani kwa kushindwa kufanya majukumu yao na kuharibu majukumu ya wananchi kushindwa kufanya kazi zao huko''

“Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na watu wachache; suala la NIDA linaenda polepole sana. Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima"

Kuhusu wakulima na wafanyabiashara, Rais amesema:

“Wanaofanya biashara ndogondogo nilishasema wasionewe ndiyo maana nilitoa vitambulisho. Nilisema mfanye biashara mahali popote lakini sikusema wapiga debe na wazuluraji waendelee kuzulura tu, kuna sheria na mimi nimeapa kulinda sheria"

“Nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha”

‘’Morogoro Ilikuwa ni mmoja kati ya mikoa muhumu sana katika uzalishaji. Viongozi wa Morogoro mukawahamasishe watu kufanya kazi ili mkoa uendelee na sifa yake ya siku zote’’

"Ukiona wengine wachache wanalalamika bei ya mahindi iko juu, najua wakulima wanashangilia, na nataka wakulima washangilie zaidi,tulizungumze hili wazi kwa watanzania wote,ukiona mahindi yako juu nenda kalime yako ya bei ya chini biashara hii lazima iwe huru"

“Wana Morogoro JPMMorogoro “Wana Morogoro nataka mtunze amani, navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kulinda amani yetu, kila mtu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi”

Kuhusu kamatakamata ya wazururaji, Rais amesema:

''Wapo wanaokamatwa kwa kosa la uzururaji na wanapopelekwa mahakamani wanashindwa. Kwanini wasishinde kule mahakamani kwamba siyo wazururaji? Wapo waliojitetea mahakamani wakashinda, sasa hao waliofungwa kwa uzururaji munataka niwarudishe?''

''Wale wanaofanya biashara ndogondogo wala wasionewe ndiyo maana nikatoa vitambulisho. Sikusema wapiga debe, wazururaji waendelee kuzurura tu – kuna sheria na mimi nimeapa kulinda sheria.''

''Niviombe vyombo vya usalama vinavyo-deal na wazururaji, wasiwaonee watu kwa kuwashitaki kama wazururaji wakati wana kazi zao. Haya ya uonevu yasiwepo.''

‘’Wale ambao siyo wazururaji musiwaonee, muwaache wafanye kazi zao.''

AKIWA WILAYANI GAIRO


Akiwa Gairo, Rais Magufuli amechangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya kujenga maabara ya Shlue ya Sekondari Sekwawa baada ya kaka Mkuu wa shule hiyo Athumani Saidi Omari kufikisha ombi la kuongeza ukubwa wa maabara hiyo ambayo amesema haitoshi.

‘’Changamoto kubwa inayaotu-cost wanafunzi wako ni maabara haitoshi’’, alisema Kaka Mkuu huyo

Rais Magufuli: ‘’Nitachangia milioni tano kama mchango wa kujenga maabara; nakabidhi milioni tano kwa ajili ya ujenzi, ikiliwa na nyie mujiandae kuliwa’’

Mkuu wa Wilaya Gairo: ‘’Hakuna mahakama ya wilaya, wanaenda Kilosa, zaidi ya kilomita 100. Hakuna ofisi ya Mkuu wa Wilaya, nimejishikiza katika ofisi za Mji Mdogo. DAS ana-share ofisi na Afisa Tarafa.''
 
Naomba nitoe ushauri kuhusu vitambulisho vya taifa.hao nida ilitakiwa wawepo kila wilaya na ofisi za kudumu ambozo hizo office inatakiwa ziwe na kila kitu kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho na sio nida wawe wanatembelea watu hapana.nchi zote ndio wanafanya hivyo.
 
Kiongozi!!! habari iongezee nyama, Mh Rais John Pombe Magufuli yupo Ikulu? Na tukumbushe jina la huyo Mkurugenzi wa NIDA.
 
Kama kuna taasisi ambayo ni ya ovyo tokea tupate uhuru basi ni awa nida watu wamejiandikisha toka 2016 mpaka leo hawana vitambulisho kama wewe sio mfanyakazi au mwanafunzi wa chuo kupata kitambulisho ni mziki najiuliza hivi hakuna wanavyuo au wafanyakazi wasio watanzania?
 
Nilisema kuhusu hili la Nida Juzi tu hapo na leo Rais ameona uozo unaoendelea,
Pale Nida ni wapigaji tu

 
Back
Top Bottom