Rais Magufuli, hili la Kangi Lugola hujatenda haki. Sheria ya Uhujumu Uchumi inawahusu wananchi tu?

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,933
Kwa Masikitiko Makubwa Kabisa!

Japo Waziri wa Mambo ya Ndani aliamua kujitoa akili na kuonesha Immaturity mbele ya kadamnasi kwa kuongea vitu ambavyo kimsingi alikuwa akijielewa mwenyewe.

Hata hivyo, halikumzuia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Rais Magufuli kuzungumza madudu ya Wizara ya Kangi.

Sitting Allowance dola 800, plus perdiem, en plus tiketi za ndege pamoja na refreshment;

Sambamba na hilo kilichosainiwa kwenye Mkataba wa Maridhiano (MoU) ni kuwa hata mkataba ukivunjwa lakini huduma ambazo zimeshaanza kutolewa basi zitaendelea kutolewa kwa kipindi chote.

Aidha, Thamani ya Mkataba ni zaidi ya 1T.

Je huyu Waziri, Naibu Waziri, Katibu, Kamishna wa Zima Moto pamoja na Maafisa wa Mwanasheria Mkuu ambapo Mikataba yote yenye thamani kubwa inayohusu Manunuzi ya Umma lazima ipite kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya kuhakikiwa terms and conditions ndio isainiwe , je wanapaswa kweli kuendelea kuwa Uraiani?

Nilitegemea kuona Gari la Magereza likimbeba pale pale bwana Kangi pamoja na timu yake kuwapeleka mahabusu.

Ukweli , Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa hii tumbua tumbua bila ya hatma ya kisheria juu ya hawa watu kujulikana inakuwa haisaidii. Na ndio maana haya matukio hayaishi. Kwa sababu hakuna liquidated damage upon specific breach pindi wakifanya madudu.

Wizara imekiuka Public Procurement Act ya Mwaka 2011 reads together with its Regulation ya Mwaka 2013 , following its amendment ya Mwaka 2016 !

Hivyo, ana sababu zote kuwa punished kisheria yeye na timu yake wakalale mahabusu; tofauti na hapo hakuna haja ya tumbua tumbua.

Tunataka kuona hawa watu wakichukuliwa hatua za kisheria kama ifuatavyo;

1. Kwenda Mahabusu
2. Kuchukuliwa Hati ya kusafiria
3. Freeze Akaunti zao zote
4. Filisi mali zao zote
5. Wanyongwe kama wafanyavyo China.

Sitting Allowance dola 800: Halafu still tunasikia hali mtaani ni ngumu, watu hawana hela, kumbe fedha zipo kwa wachache.

Hili pia ni lako ewe Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa kujitafakari kuwa ni kweli Ufisadi kwenye Taasisi za Umma umekwisha au unafanyika lakini ni kwa kificho?

Mwisho, zifuatazo ni taasisi ambazo unatakiwa kuwaambia vijana wako wazitembelee hizi taasisi kwa uchunguzi zaidi;

1. PPP project ya Mwendokasi
2. NSSF na nyumba za Kijichi, tunajua Serikali ilikuwa na Hisa ndogo katika mradi huu, lakini cha kushangaza Serikali ndio iliyotoa Bilions of money kuliko kampuni Binafsi
3. Bohari Kuu ya Dawa chini ya Wizara ya Afya- Tulisoma Ripoti ya CAG inayoeleza upotevu mkubwa wa pesa za Dawa za wànanchi pasipokuwa na nyaraka yakinifu.Hapa rushwa ipo mno
4. NIDA ikiwa ni pamoja na Utendaji wao
5. TTCL hawa hasa kwenye huduma zao na kuna viashiria vya Rushwa vingi sana
6. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
7. Bodi ya Mikopo

Asante!
 
Ni kweli kabisa mfano bodi ya mikopo mkurugenzi wa repayment anact huu mwaka wa nne na anapiga pesa vibaya sana kupitia ma meneja wa kanda yani kwa mwezi anakusanya si chini ya milioni 20
 
Mie naona General mstaafu ndio kachoma utambi, inaonekana kumetokea sintofahamu, General kampandia mkuu ofisini kamwaga kilakitu na resignation juu, labda alimtishia kuwa anarudi lugalo, akaona isiwe tabu, manake yeye kalamba ubalozi.

Kangi inaonekana kapigwa katafunua, yaani nyani usimwangalie usoni, hakutegemea ataenda kukumbana na kadhia ile asingeenda mkutanoni.

Romania niwatengenezaji wa magari mazuri ya zimamoto aina ya Magnus pia ndio watengenezaji wa bidhaa Bora za kuzimia Moto. Chamsingi mkataba upitiwe upya nakuweka mambo sawa.

Nashauri hapo mambo ya ndani atafute jembe jingine kutoka jeshini, mie napendekeza major general Makakala balozi wetu Zimbabwe.
 
Hii ni kweli; Lakini inasemekana pia Mwanasheria Mkuu alivyorudi ndio aka review zile kopi ya Mikataba, alivyoona hivyo ikabidi na yeye ajisalimishe asije kukubwa na balaa.

Cha kushangaza Rais anasema Maafisa wa Mwanasheria Mkuu waliopitisha huo Mkataba eti wajitafakari, hawa watu ni wa kwenda Jela straight.

Kuna asilimia kubwa taarifa zimeanza kutoka kupitia ofisi ya AG ( Mwanasheria Mkuu) wale vijana wa pale wanatabia sana ya kutoa siri za mikataba ya watu, na wengine hupeleka taarifa kwa Suppliers. Pale pia pachunguzwe sijui kama
Vile Vi Afisa vinajua kanuni za Utumishi wa Umma.
 
Rais amemsimasha Kangi Lugola na Andengenye kwa tuhuma za kusaini mkataba wa hovyo!! Je Takukuru hamuwezi kuwafungulia mashtaka ya kuhujumu uchumi wahusika?

Au ndio kusema vyombo vyetu vya dola vimezoea kufanya kazi kwa maelekezo na sio weledi. Hii ya kusemwa na Rais ilikuwa inatosha kabisa kuwachukulia hatua wahusika. Nami nawaomba TAKUKURU mjitasimini kama hamutawachukulia hatua hawa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais amemsimasha Kangi Lugola na Andenye kwa tuhuma za kusaini mkataba wa hovyo!! Je Takukuru hamuwezi kuwafunguli mashitaka ya kuhujumu uchumi wahusika? au ndio kusema vyombo vyetu vya dola vimezoea kufanya kazi kwa maelekezo na sio weledi!! Hii ya kusemwa na Rais ilikuwa inatosha kabisa kuwachukulia hatua wahusika! Nami nawaomba Takukuru mjitasimini Kama hamutawachukulia hatua hawa watu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndio lishafikia tamati.... Tugange yajayo

Jr
 
Takukuru wao walikuwa wapi mpaka TISS ndio wamtonye magu.TAKUKURU wafanye kazi pia kwa kushirikiana na vyombo vingine ili watu kama hawa wapatikane.Kwa kawaida TAKUKURU ilibidi ndio wawe wa kwanza kuwashughulikia hawa jamaa lakin je nani awezaye kuwagusa wateule wa Mteule?
Magari binafsi ya RCDSM thamani yake ni zaidi ya 1Bilion za kitanzania lakin PccB huwezi kuona wakimgusa.Huu ni unafiki na unatukwamisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom