Rais Magufuli, hebu liangazie macho hili la Ziwa Nyasa!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
Serikali yako ituhakikishie wananchi bado Ziwa Nyasa lipo na Tanzania inayo haki yake.

Uliapa kulinda Mipaka ya Tanzania. Kimya chako wakati majirani wakizidi kuuaminisha ulimwengu kuwa sisi hatuna chetu si sawa.

5cbaf421-ecb1-42f4-a1a8-fb0d162026cd.jpg
 
Hawa wanasiasa wa Malawi uchaguzi wao ukikaribia ajenda inakuwa ni kuliteka ziwa la Nyasa kampeni zao zikiisha wanakaaga kimya utsema sio wao,ila mimi naamini iko siku watatu test.
 
Serikali yako ituhakikishie wananchi bado Ziwa Nyasa lipo na Tanzania inayo haki yake.

Uliapa kulinda Mipaka ya Tanzania. Kimya chako wakati majirani wakizidi kuuaminisha ulimwengu kuwa sisi hatuna chetu si sawa.

View attachment 860920
Hili ni tatizo la kihistoria toka mkoloni, Wenzetu malawi wamekuwa wakiwafundisha watoto wao hivyo na sisi tukifundishwa hivi.
International Map nyingi zilikuwa zikikubaliana na ramani tuliyo nayo Tanzania.
Ni busara kidogo tu na muda mwingi unahitajika kuweka sawa jambo hili
 
simple logic ili ziwa liwe la kwao lote inatakiwa songea yote iwe sehemu ya malawi na baadhi ya maeneo mengine ya tz yanayo zunguka ziwa hilo. VINGINEVYO HAYO MAJI LAZIMA TUYAGAWANE NCHI ZOTE MBILI
 
Hawa wamalawi "wakileta fyoko fyoko" tutabinafsisha ka nchi kao kote, tukafanye mkoa wetu tu.
 
Natamani mkuu aongee juu ya hili, maana wamalawi watapata cha kuandika kwenye magazeti yao na bila shaka hawatazungumzia tena hili.. Wakileta fyoko fyoko tunapiga na Malawi inakuwa Tanzania mnasemaje wananchi..
 
Hii habari ya Tanganyika kutokuwa na chake kwenye ziwa Nyassa nilianza kulikisikia miaka ya sitini nikiwa bado mtoto mdogo, lakini niliweza kuelewa kuwa kuna fukuto la vita kati yetu na Malawi, mwanzoni kabisa Kamuzu Banda Hastings akituhumiwa kutumika na makaburu wa Afrika kusini dhidi ya nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru ikiwemo Tanzania.

Msingi wa mgogoro katika ziwa Nyassa unatokana na kushindwa vita kwa ujeremani ambaye alikuwa mtawala wa Tanganyika na hivyo hata baada ya Tanganyika kupata uhuru hakukuwepo mazungumzo kuhusu mpaka huo hadi wakati wa utawala awamu ya nne.Kimsingi tulirithi Tanganyika iliyoshindwa vita ikiwa na mipaka tunayoijua sisi wakati wenzetu Malawi wanatambua mipaka ya mkoloni wao.

Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na Rais Kamuzu Banda na hivyo hakukuwa na namna yoyote ya hawa wawili kukaa na kujadili kuhusu matokeo ya vita vya wakoloni wetu zaidi ya kutuhumiana tu. Suala hili linahitaji ufumbuzi wa kidiplomasia na mazungumzo yanayohusisha umoja wa Mataifa, umoja wa Afrika,Malawi na Mozambique na ni vyema ukatatuliwa sasa badala ya kungoja mpaka tukunjane mashati.
 
Akili yangu wakati mwingine in kama ya Magufuli. Sipendi mambo ya kubembeleza...kama hawataki piga wote chukua ziwa na nchi yao
 
Hii habari ya Tanganyika kutokuwa na chake kwenye ziwa Nyassa nilianza kulikisikia miaka ya sitini nikiwa bado mtoto mdogo, lakini niliweza kuelewa kuwa kuna fukuto la vita kati yetu na Malawi, mwanzoni kabisa Kamuzu Banda Hastings akituhumiwa kutumika na makaburu wa Afrika kusini dhidi ya nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru ikiwemo Tanzania.

Msingi wa mgogoro katika ziwa Nyassa unatokana na kushindwa vita kwa ujeremani ambaye alikuwa mtawala wa Tanganyika na hivyo hata baada ya Tanganyika kupata uhuru hakukuwepo mazungumzo kuhusu mpaka huo hadi wakati wa utawala awamu ya nne.Kimsingi tulirithi Tanganyika iliyoshindwa vita ikiwa na mipaka tunayoijua sisi wakati wenzetu Malawi wanatambua mipaka ya mkoloni wao.

Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na Rais Kamuzu Banda na hivyo hakukuwa na namna yoyote ya hawa wawili kukaa na kujadili kuhusu matokeo ya vita vya wakoloni wetu zaidi ya kutuhumiana tu. Suala hili linahitaji ufumbuzi wa kidiplomasia na mazungumzo yanayohusisha umoja wa Mataifa, umoja wa Afrika,Malawi na Mozambique na ni vyema ukatatuliwa sasa badala ya kungoja mpaka tukunjane mashati.
Mjerumani hakuwahi kumiliki sehemu ya Ziwa Nyasa, waingeleza walikuwa wamesh mtangulia ktk harakati za Ku claim umiliki. Mwingeleza alimiliki ziwa lote. Baadaye aliingia kwenye mazungumzo na Wareno, wakabadilishana sehemu ya ardhi ya Mozambique kwenda Malawi, na Malawi akatoa sehemu ya ziwa. Kwa upande Wa Tanzanyika hill halikufanyika maana Mara ya mjerumani kuondolewa Tanganyika, mwingeleza alipewa usimamizi akitumai atapewa Tanganyika kuwa koloni lake. Na alianza jitihada za kuunganisha mambo ya utawala Wa sehemu ya mkoa wa Mbeya na Kalonga. Alipokataliwa mwaka 1945 kupewa Tanganyika kama koloni laki alighafirika na kusitisha jitihada na kuunganisha sehemu ya mkoa Wa Mbeya na Kalonga. Hivyo akabakisha mipaka kama ilivyoachwa na Wajerumani
 
Ziwa Nyasa Kwa Malawi ni kete ya kushinda uraisi na ubunge kwao nikama rushwa Kwa sisiemu wakati wa uchaguzi wana ilaani kumbe unafiki mtupu
 
Hawa wanasiasa wa Malawi uchaguzi wao ukikaribia ajenda inakuwa ni kuliteka ziwa la Nyasa kampeni zao zikiisha wanakaaga kimya utsema sio wao,ila mimi naamini iko siku watatu test.
Siku wakitest tutawasha mitambo ndio watajamba cheche na kunya moto
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom