Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili ni tatizo la kihistoria toka mkoloni, Wenzetu malawi wamekuwa wakiwafundisha watoto wao hivyo na sisi tukifundishwa hivi.Serikali yako ituhakikishie wananchi bado Ziwa Nyasa lipo na Tanzania inayo haki yake.
Uliapa kulinda Mipaka ya Tanzania. Kimya chako wakati majirani wakizidi kuuaminisha ulimwengu kuwa sisi hatuna chetu si sawa.
View attachment 860920
hawez zungumzia hilo swala. na akizungumzia tafadhali uje unikumbushe kupitia uzi huu!Mwamba anakuja huko tulieni
kwa nini hawezi kuzungumzia hilohawez zungumzia hilo swala. na akizungumzia tafadhali uje unikumbushe kupitia uzi huu!
Mjerumani hakuwahi kumiliki sehemu ya Ziwa Nyasa, waingeleza walikuwa wamesh mtangulia ktk harakati za Ku claim umiliki. Mwingeleza alimiliki ziwa lote. Baadaye aliingia kwenye mazungumzo na Wareno, wakabadilishana sehemu ya ardhi ya Mozambique kwenda Malawi, na Malawi akatoa sehemu ya ziwa. Kwa upande Wa Tanzanyika hill halikufanyika maana Mara ya mjerumani kuondolewa Tanganyika, mwingeleza alipewa usimamizi akitumai atapewa Tanganyika kuwa koloni lake. Na alianza jitihada za kuunganisha mambo ya utawala Wa sehemu ya mkoa wa Mbeya na Kalonga. Alipokataliwa mwaka 1945 kupewa Tanganyika kama koloni laki alighafirika na kusitisha jitihada na kuunganisha sehemu ya mkoa Wa Mbeya na Kalonga. Hivyo akabakisha mipaka kama ilivyoachwa na WajerumaniHii habari ya Tanganyika kutokuwa na chake kwenye ziwa Nyassa nilianza kulikisikia miaka ya sitini nikiwa bado mtoto mdogo, lakini niliweza kuelewa kuwa kuna fukuto la vita kati yetu na Malawi, mwanzoni kabisa Kamuzu Banda Hastings akituhumiwa kutumika na makaburu wa Afrika kusini dhidi ya nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru ikiwemo Tanzania.
Msingi wa mgogoro katika ziwa Nyassa unatokana na kushindwa vita kwa ujeremani ambaye alikuwa mtawala wa Tanganyika na hivyo hata baada ya Tanganyika kupata uhuru hakukuwepo mazungumzo kuhusu mpaka huo hadi wakati wa utawala awamu ya nne.Kimsingi tulirithi Tanganyika iliyoshindwa vita ikiwa na mipaka tunayoijua sisi wakati wenzetu Malawi wanatambua mipaka ya mkoloni wao.
Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na Rais Kamuzu Banda na hivyo hakukuwa na namna yoyote ya hawa wawili kukaa na kujadili kuhusu matokeo ya vita vya wakoloni wetu zaidi ya kutuhumiana tu. Suala hili linahitaji ufumbuzi wa kidiplomasia na mazungumzo yanayohusisha umoja wa Mataifa, umoja wa Afrika,Malawi na Mozambique na ni vyema ukatatuliwa sasa badala ya kungoja mpaka tukunjane mashati.
Wewe ni jukumu lako kumsaidia. Siyo kejeli. Una wajibu huoMagufuli anahitaji msaada mkubwa sana kutatuwa hili, kwenye diplomasia ana chini ya sifuri
Siku wakitest tutawasha mitambo ndio watajamba cheche na kunya motoHawa wanasiasa wa Malawi uchaguzi wao ukikaribia ajenda inakuwa ni kuliteka ziwa la Nyasa kampeni zao zikiisha wanakaaga kimya utsema sio wao,ila mimi naamini iko siku watatu test.