Rais Magufuli, haya ya Kilango ni madhara ya kuteua waliokatawaliwa na wananch

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Alichokifanya Magufuli ni kudhibitisha madai ya muda mrefu ya vyama vya upinzani kuwa ni makosa kumteua mtu aliyekataliwa na wananchi kwa kushindwa "kudeliver".

Kutumbuliwa kwa Anne Kilango Malecela ni heshima kubwa kwa wananchi wa Same Mashariki waliomktaa kwenye sanduku la kura mwaka jana na kumchagua mama Kaboyoka (CHADEMA). Maana yake ni kwamba wanancahi wa Same Mashariki waliugundua udhaifu wa Mama Kilango kabla washauri wa Rais hawajauona.

Haiwezekani mtu aliyekataliwa na wananchi kwa kushindwa kuwajibika apewe mkoa au wilaya kuongoza. Wapinzani wamepiga kelele miaka mingi wakisema kumteua mtu aliyekataliwa na wananchi ni kuwatukana wananchi hao lakini serikali iliziba masikio.

JPM nae hakuamini hiyo falsafa kwa maneno. Akataka afanye experiment ajue kama madai hayo ni kweli au lah. Si unajua huyu ni "Mkemia" kwahiyo kila kitu anaprove.? Akaamua kuprove kwa kuwateua walewale waliokataliwa na wananchi. Sasa ameanza kupata majibu ya "experiment" yake.

Nategemea kabla hajatoka maabara (Ikulu) specimen zifuatazo zitakuwa "zimeshareact" kweny chemichals za "Pombe" na kuungua vibaya;

1. Godfrey Zambi – huyu alikataliwa na wananchi wa Mbozi, Wakamchagua Pascal Haonga (CHADEMA). Lakini JMP akamfanyia experiment na kumteua kuwa RC Lindi. Soon tutaona "reaction".

2. Dkt. Steven Kebwe – Huyu alikataliwa na wananchi wa Serengeti wakamchagua Mwal.Chacha Ryoba (CHADEMA), lakini JPM kuaamua kumfanyia experiment kwa kumpeleka Morogoro. Subiria "chemical reaction" soon.

3. Aggrey Mwanri – huyu alikataliwa na wananchi wa Siha na wakamchagua Dr.Godwin Mollel (CHADEMA). Lakini JPM kaamua kumtest kwa kumpa uRC Tabora. Hapa subiria "Acid-Base reaction".

4. Magesa Mulongo – huyu hakugombea popote lakini hana sifa ya uongozi. Kama umefanya nae kazi utaelewa nachosema. Ni mbabe, ana dharau, na majivuno. Alipigana na Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza kwenye kikao cha Kamati ya ulinzi na usalama lakini Katibu Tawala akafukuzwa kazi yeye akaachwa.

Alipopangiwa kuwa RC Mwanza alikataa nyumba aliyokua akikaa mtangulizi wake Ernest Ndikilo kwa madai kuwa haina hadhi yake. Kwahiyo akaenda kupanga Capripoint kwa gharama ya Shilingi milini 7.8 kwa mwezi zilizokua zinalipwa na serikali. JPM alipoingia madarakani akaogopa kutumbuliwa akarudi kwny nyumba ile aliyoikataa na hapa ndio ukaanza ugomvi kati yake na Katibu Tawala.

Kila alipopita huyu jamaa ameacha migogoro. Arusha hawataki kumuona hata kumsikia. Huwa sielewi ilikuaje akapenya kwenye mchujo wa JPM. But haihitaji degree kujua kwamba yupo "maabara" anapimwa. Kapelekwa kwenda kuwa RC mkoa wa Mara, but very soon tegemea kusikia "Solid state reaction" kutoka Musoma.
 
Back
Top Bottom