Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Rais Magufuli,kama Marais wote wanne wa Tanzania waliomtangulia,ana matamanio yake. Matamanio yake ameyaweka kwenye malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Kama Rais,kiongozi mkuu wa Serikali,anasuka mipango ya kuyafikia malengo aliyojiwekea.
Pamoja na uwepo wa Ilani ya chama chake cha CCM,Rais Magufuli ana vipaumbele vyake kulingana na anachotaka kufanya na kukiacha kwa wananchi hata atakapotoka madarakani muda wake utakapoisha.
Rais Magufuli ana aina yake ya kutafakari,kuamua na kufanya jambo. Hapo ndipo hasa humtofautisha na mtangulizi wake yeyote. Hata watangulizi wake wote wanne nao wanatofautiana kati yao katika kutafakari,kuamua na kufanya jambo
Rais anapoweka njia ya kupita,wateule wake wote hufuata humo. Hakutarajiwi mteule wake yeyote kwenda kinyume au pembeni ya njia hiyo kwakuwa ndiyo njia ya Rais mwenyewe,ambaye atajibu kwa wananchi na atawaachia cha kuwaachia.
Yeyote atakayekuwa na makandokando au kujifanya mjuaji atakwenda na maji. Kwa maana,makandokando na ujuaji humtoa mhusika kwenye njia ya Rais. Rais hawezi kuruhusu mijadala badala ya wateule kutekeleza majukumu yao kulingana na malengo ya Rais
Ndiyo kusema,Rais hana mteule anayempenda kuliko wengine. Pia,hana mteule anayemchukia kuliko wengine. Atayapenda au kuyachukia maneno na matendo yanayopimwa kulingana na njia aliyoichonga kupitwa na Serikali yake. Kipimo kitabakisha au kutoa yeyote.