Rais Magufuli, watumishi wa Umma ambao hatukupandishwa madaraja hamjatutendea haki

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Mh Rais tunakuomba sisi watumishi wa umma ambao hatukupandishwa madaraja sababu tulienda masomoni kwa kweli hamkutendea haki.

Mh Rais kwenda masomoni ni kuongeza ufanisi kazini na kuinua utendaji kazi si dhambi.

Masomoni hatukwenda kuzurura bali kuongeza ujuzi maarifa ili kuifanyia kazi serikali ili kuliletea maendeleo Taifa letu na pia kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Asilimia kubwa wa watumishi tulioenda masomoni hatukugharamikiwa na Halmashauri wala serikali kuu bali sisi wenyewe na unavyojua mishahara yetu ndo tulikopa ili kulipa ada,hostel, stationary na chakula.

Hivyo tulikopa ili kugharamikia masomo ya chuo hivyo baada ya kutoka chuo Taasisi za kifedha wanaendelea kutukata fedha zao

Mh Rais ukumbuke sisi tunaojiendeleza tunatokea familia masikini ndo maana hatukwenda masomo juu moja kwa moja kipindi tukiwa wanafunzi wa Olevel na Advance kwa sababu wazazi wetu au walezi wetu hawakuwa na uwezo badala yake wakatutaka twende chuo badala ya masomo ya juu maana hawakuwa na uwezo.

Mh Rais watumishi wengi wa umma tunatokea kwenye familia tegemezi ,kutopandishwa madaraja inatuumiza mnooo.

Mh Rais kutopandishwa madaraja ,sawa tunaenda kazini lakini tuna kinyongo,ghadhabu,yaani ile ari ya kufanya kazi hatuna.

Tunakuomba mh Rais swala hili mliangalie upya,tunaumia si mchezo.
 
Acha kulalamika hebu jitolee kuijenga nchi yako. Fanya kama ni njia ya kujitolea kuijenga taifa hutakaa na kinyongo tena
 
DJ lete mambo in JK voice, "wacha waseme ccm ina wenyewe"

Ukikubali kula, kubali nakuliwa

Kiduma chama cha mapinduzi.
 
Hao wafanyakazi wengi au niseme wote wamenenepa yaani sijui ni kula au ni kutokufanya mazoezi, sijui wanakula nini.
 
Raisi aki soma huu uzi atakasirika sanaaa....alisha sema hapa Kazi tu.

Kama hautaki Kazi acha hakuna anaye kulazimisha alisikika mataga mmoja mm nimemnukuu tu.
 
Nani kapandishwa sasa
Jamaa analalamika baada ya kwenda masomoni! Si bora hata yeye alipata muda wa kwenda ku refresh mind!! Hivi hafahamu hata sisi tuliobaki tangu enzi Rais ni Kikwete, bado tunaishi kwa madaraja na mishahara ile ile!

Halafu eti Nchi ina Rais! Rais gani huyu asiye jali haki za wengine!! Muda wote anajijali yeye mwenyewe, wasaidizi wake, ndugu zake na nyumbani kwake!
 
Tunabaki tunamshangaa badala aunganishe kilio kilichopo anakuja na engo tofauti
 
Hao wafanyakazi wengi au niseme wote wamenenepa yaani sijui ni kula au ni kutokufanya mazoezi, sijui wanakula nini.
hujawahi kuwaona wanajeshi wenye vitambi pamoja na kwata kibao.ukisha adamp mazingira ,stress zinatoka,body mechanism zina operate under balanced.lazma kitambi kitoke hata Kama umezungukwa na changamoto.
 
Back
Top Bottom