Rais Magufuli hali ya maisha ni ngumu sana, tuonee huruma

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda.

Ila hali yetu wananchi ni mbaya sana. Tunaamka asubuhi hatujui kama tutakula au vipi. Tukifungua biashara zinakufa, kila tunachojaribu hakiendi.

Hivyo wewe kama mkuu angalia namna ambavyo utalegeza ili mzunguko wa pesa uongezeke mitaani. Sio kwamba hatutaki kazi bali mzunguko wa pesa ni hakuna kabisa.
 
Hapo sasa atujawekwa lock down hivi ingekuwaje.

Kipindi hiki cha corona ni dhahiri uchumi wa dunia utatetereka sio tanzania tu bali hata nchi zilizoendelea.
kikubwa ni dunia sasa ifunguliwe maisha yaendelee ili ku stemulate tena uchumi upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kafungua viwanja vya ndege subiri uone lakini kwa ugonjwa wa covid-19 watu wanaishi kwa kujihami hakuwezi kuwa na mzunguko wa pesa lakini pia ni aina ya uchumi ambao tunaenda nao nadhani umefeli tulihitaji uchumi ambao huinua kipato cha mtu mmoja mmoja 'Welfare ecomy'
 
Out of point. Kuwa serious na maisha. Mama ntilie, wauza maandazi na machinga wanalia njaa.

Njaa hiyo ni mtambuka wa sera mbovu za serikali za uchumi, biashara, kilimo, masoko na kodi kama Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo anavyobainisha ktk video clip post # 9 hapo juu.

Hivyo wananchi mtaani lazima waione hali hiyo ngumu ktk ngazi ya familia / kaya.
 
Hata kabla ya Corona hali ya mzunguko wa pesa ulikuwa mbaya.
Shida ni mmoja miradi mikubwa ya Magufuli inayotekelezwa na makandarasi wa nchi za nje.Hao makandarasi wageni pesa yote wanapeleka kwao.
Na hao wafanyakazi watanzania wanalipwa mishahara midogo sana na makampuni hayo ya kigeni.
Magufuli atafute vianzo vingine lakini miradi mipya wapewe wazawa.
 
Iyo miladi mikubwa inahitaji wataalamu na vifaa vya kisasa, inahitaji mtaji mkubwa, ina hitaji uzoefu wa kutosha. Hakuna serikali duniani ingependa miradi mikubwa tena inayotumia fedha nyingi kupewa kampuni za kigeni. Tatizo kampuni zetu zunashindwa kwenye zabuni kutokana na mapungufu niliyo ainisha hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kabla ya Corona hali ya mzunguko wa pesa ulikuwa mbaya.
Shida ni mmoja miradi mikubwa ya Magufuli inayotekelezwa na makandarasi wa nchi za nje.Hao makandarasi wageni pesa yote wanapeleka kwao.
Na hao wafanyakazi watanzania wanalipwa mishahara midogo sana na makampuni hayo ya kigeni.
Magufuli atafute vianzo vingine lakini miradi mipya wapewe wazawa.
Hao wazawa wanao uwezo wa kufanya mradi kama wa daraja la Busisi kwenda Kigongo. Mbona wakati wa Mkapa kulikuwa na miradi mingi na ilijengwa na wageni na mzunguko wa pesa ulikuwepo? Yeye aangalie Fiscal policies nzuri ili pesa ziwafikie wananchi.
 
Tuvumilie miradi ikiisha hela itakuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu utakuta wananchi wanaisifia na kuipongeza serikali kwa miradi mikubwa ya Ndege, SGR reli, madaraja ya baharini , flyovers, Majengo ya hospitali bila vifaa-tiba wala dawa huku pia wakilia kuwa hali ya maisha ni ngumu sana pesa hakuna.

Hii ni nchi yenye raia wa ajabu.

CCM Oyee !
 
Piga moyo konde kwa kumwoba MUNGU na zidi kujituma pia epuka kuwa mtu wa lawama kiongozi

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Kaka nime soma comment yako. Kimsingi nikushauri. Mimi ni mtaalam wa Biashara. Usifungue Biashara kwa kufuata mkumbo.

Kabla ya kuanzisha Biashara Fanya Utafiti kwanza. Angalia soko na uhitaji wake. Je!Biashara ninayotaka kuanzisha inauhitajika Kiasi gani?

Unafanya Tafiti ndio unaanzisha Biashara. Pia unaangalia Biashara Ambayo Inamzunguko wa kila siku kama chakula. Na bidhaa za matumizi ya kila siku.

Ukizingatia haya Huta feli hata siku Moja MKUU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idugunde,

Serikali ya CCM ilivyoharibu uchumi wa nchi, usiombe hisani toka kwa CCM bali fanya kweli kupitia sanduku la kura kwa kuchagua chama tofauti na CCM

December 2019
Zitto akiongea na wananchi Akichambua hali ya uchumi kuelekea uchaguzi 2020

 
Back
Top Bottom