Rais Magufuli: Hali kwa sasa ipo vizuri na Corona inapungua. Wanafunzi wa Form VI na Vyuo vyote kufunguliwa 01 Juni 2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
30,033
2,000
Karibu

Wageni wameshawasili katika sherehe hii ambayo wateule kadhaa wataapishwa akiwemo Naibu waziri wa afya, Katibu tawala mkoa wa Pwani Mkurugenzi wa Takukuru na mabalozi.

Rais Magufuli ameshaingia ukumbini tayari kuanza kuwaapisha wateule wake.=====
Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa

Prof. Kabudi - Canada yaipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua dhidi ya CoronaVirus na wameahidi kusaidia kusaidia kwenye swala la elimu

Waziri Wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada. Canada imetupongeza kwa namna ambavyo tumepambana na Covid19. Wameahidi watatisaidia katika maeneo ya elimu na afya kwa kadiri mahitaji yetu yatakavyokuwa.

Nilimsisitizia Waziri yule kuwa sisi watupe pesa na tutajua ni maeneo gani katika nchi hii tutazipeleka, katika kuimarisha uchumi na katika kupambana na maradhi haya.

Juzi pia niliongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umeamua kutoa Dola milioni 38 ambazo zitakuja Tanzania kutusaidia katika maeneo mbalimbali baada ya hili janga la Coronavirus.

Pia niliongea na Balozi wa Sweden kwa njia hii hii ya mtandao. Sweden wataongeza Dola milioni 20 katika bajeti ya elimu na Dola milioni 10 kwenda TASAF

Ummy Mwalimu - Tulijiandaa kuchukua uwanja wa sabasaba ili kuwaweka wagonjwa wa corona lakini sasa wagonjwa wamepungua kwa hiyo uwanja umerudishwa

Suleiman Jaffo - Nyungu season two inaanza Jumatatu... pia tuwaambie watalii kuwa, wanakaribishwa Tanzania wakifika wanapewa zawadi ya nyungu

Magufuli - Corona bado ipo, imepungua ni kweli lakini tuendelee kuchukua tahadhari

- Msikubali vifaa vya corona vinavyogawiwa na taasisi mbalimbali, kama ni kupokea kifaa cha kupambana na corona, kipitie Wizara ya Afya na kiwe checked.

- Katika michango hii unaweza kuletewa hata barakoa zenye corona kwa kuwa trend yetu iko vizuri, vya bure ni vibaya

- Mtu akileta kifaa kikichunguzwa kikakutwa na korona apewe kesi ya jinai hata ya kuua kabisa

- Vyuo vikuu vyote vitafunguliwa tarehe 1/6/2020

Vijana wa kidato cha sita watarudi shuleni 1/6/2020, pia iandaliwe crash program ili isiharibu utaratibu wa wao kuingia chuo kikuu,

Sekondari na shule za msingi zinapewa muda wa kujitazama ila chuo kikuu wanajitambua

Michezo
- Kuanzia tarehe 1/6/2020 michezo yote ianze rasmi kuanzia ligi daraja la kwanza, taratibu za kushangilia na kushabikia zitatolewa muongozo na Wizara ya Afya

Immunity inaongezeka mtu akiwa anainteract, ukimfungia immunity inaweza kushuka kwa 30%

--
Kuanzia tar 27/28 Mei 2020 itaanza kuruhusu ndege kuingia nchini, na watalii hawatafungiwa kwa siku 14, atamuikwa na kama joto lake litakuwa chini ya ile jotoridi linalotakiwa,

Miti ya kujifukiza itolewe kama Complementary kwa watalii

Magufuli: Mungu amejibu maombi yetu.

Watakaoguswa kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili tutumie siku hizo kumshukuru Mwenyezi Mungu
 
Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
17,080
2,000
Barakoa ni muhimu sana mrembo. Usikubali kuwa kwenye public area bila ya mask 😷 popote pale in order to reduce the risk of COVID infection.
Kama kwenye public ambapo hakutakuwa na umbali kati ya watu,au nitalazimika kuongea na mtu hapo yes. Ila kama sehemu nitakeep distance mimi sivai. Binafsi nikivaa Barakoa kila nikihema ile hewa inakuwa vapor inaweka ukungu kwenye miwani yangu.

Na mimi bila miwani sioni vizuri. Kusema ukweli navaa Barakoa kwenye misongamano tu.
 
Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,798
2,000
Prof. Kabudi - Canada yaipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua dhidi ya CoronaVirus na wameahidi kusaidia kusaidia kwenye swala la elimu

Ummy Mwalimu - Tulijiandaa kuchukua uwanja wa sabasaba ili kuwaweka wagonjwa wa corona lakini sasa wagonjwa wamepungua kwa hiyo uwanja umerudishwa

Suleiman Jaffo - Nyungu season two inaanza Jumatatu,.... pia tuwaambie watalii kuwa, wanakaribishwa Tanzania wakifika wanapewa zawadi ya nyungu

Magufuli - Corona bado ipo, imepungua ni kweli lakini tuendelee kuchukua tahadhari

- Msikubali vifaa vya corona vinavyogawiwa na taasisi mbali mbali, kama ni kupokea kifaa cha kupambana na corona, kipitie wizara ya afya na kiwe checked

- Katika michango hii unaweza kuletewa hata barakoa zenye corona kwa kuwa trend yetu iko vizuri, vya bure ni vibaya

- Mtu akileta kifaa kikichunguzwa kikakutwa na korona apewe kesi ya jinai hata ya kuua kabisa

- Vyuo vikuu vyote vitafunguliwa tarehe 1/6/2020

Vijana wa kidato cha sita watarudi shuleni 1/6/2020, pia iandaliwe crash program ili isiharibu utaratibu wawao kuingia chuo kikuu,

Sekondari na shule za msingi zinapewa muda wa kujitazama ila chuo kikuu wanajitambua

Michezo

- Kuanzia tarehe 1/6/2020 michezo yote ianze rasmi kuanzia ligi daraja la kwanza, taratibu za kushangilia na kushabikia zitatolewa muongozo na wizara ya afya

Immunity inaongezeka mtu akiwa anainteract, ukimfungia immunity inaweza kushuka kwa 30%

--
Kuanzia tar 27/28 Mei 2020 itaanza kuruhusu ndege kuingia nchini, na watalii hawatafungiwa kwa siku 14, atamuikwa na kama joto lake litakuwa chini ya ile jotoridi linalotakiwa,

Miti ya kujifukiza itolewe kama Complementary kwa watalii

Magufuli: Mungu amejibu maombi yetu

Watakaoguswa kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili tutumie siku hizo kumshukuru mwenyezi Mungu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
98,458
2,000
COVID haimbukizwi kwa kupitia kinywani tu hata ukivuta oxygen kama kuna mtu aliyenayo karibu yako unaweza kabisa kuipata. Kumbuka kuna wengi wanayo lakini ni ASYMPTOM na ukiwa jirani na mtu aliyenayo huku wewe umevaa 😷 unapunguza percentage ya kuambukizwa toka 100% hadi 4% that’s HUGE. Please protect yourself and your loved ones.

Kama kwenye public ambapo hakutakuwa na umbali kati ya watu,au nitalazimika kuongea na mtu hapo yes. Ila kama sehemu nitakeep distance mimi sivai. Binafsi nikivaa Barakoa kila nikihema ile hewa inakuwa vapor inaweka ukungu kwenye miwani yangu. Na mimi bila miwani sioni vizuri. Kusema ukweli navaa Barakoa kwenye misongamano tu.
 
Top Bottom