Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Abed Kipanya
Mtela Mwampamba
Peter Kalihose
Teddy Tarimo
Kimeta Wa Mpui
Hussein H Kitambi
Grayson M Nyakarungu
Asenga Abubakar
Majina mengine ongeza wewe.
Na hii ndio maana ya shairi langu la wiki iliyo pita ambalo watu walilielewa ndivyo sivyo, kutumika kama salama, mtumiaji anaona raha lakini wewe wapata tabu kisha watupwa kama uchafu wa haja kubwa.
KILIO CHA SALAMA.
Salama ninaumia, mizigo kukubebea,
Ndani unapo ingia, na nje kujitokea,
Michubuko wanitia, mwenyewe wachekelea,
Mengi umenitendea, ukome kunitumia.
Hamu yako ulegee, na pumzi zikuishie,
Hapa pale uchezee, lengo hilo ufikie,
Natangulizwa kulee, kunako nikaingie,
Kama chuki uchukie, nataka nipotezee.
Huoni na husikii, chozi langu hulijui,
Wallahi hufikirii, kwa fujozo sipumui,
Ujuacho usanii, kulia na wako bui,
Mi' ndururu siijui, kazi kubeba madhii.
Ujue nina kilio, cha miaka si cha leo,
Wanitesa mtwangio, mawio hadi machweo,
Naomba tega sikio, waumiza mchezeo,
Kwako sina tegemeo, jalala langu fikio.
Tisa kumi sisahau, ufikapo kule juu,
Tanishika kidharau, na mate tatema, puu!
Sina thamani mdau, pamoja na kazi kuu,
Nabaki kutota tuu, nawe wakauka kau.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
call/whatspp 0622845394 Morogoro.