Uchaguzi 2020 Rais Magufuli hakumtuma mzee Aggrey Mwanry kugombea Tabora, amemstaafisha

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,432
7,055
Kuna watu ni wazito wa kuconnect dots. Ngoja tuwasaidie.

Tabora pamepata umaarufu wa mitandaoni hivi karibuni, kutokana na mbwembwe za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Aggrey Mwanry.

Umaarufu huo haukuwa na tija bali ulilenga kumjenga mwanasiasa huyu mkongwe kuja kugombea tena ubunge. Aliona akigombea Tabora itamgeuka, akahamisha goli makusudi ili kuficha dhamira yake. Siasa za hivi zinaboa

Ndio maana, Rais akaamua kutengua uteuzi wake na kumsitiri kwa kusema amestaafu. Ukweli ni kwamba alimshtukia kuwa naye ni miongoni mwa viongozi wenye tamaa. HARIDHIKI. Akamuweka kando

Tabora kuna vijana ni watendaji na wamehamasisha maendeleo ya kweli kwa muda mrefu. Umaarufu kwao si kitu, bali utendaji wenye impact

Leo nimefurahi kuona mmojawapo wa watu ninaowafahamu kuamua kujitokeza front kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uwakilishi bungeni. Angalau maigizo yatapumzika.

Huyu chalii amekuwa Mwenyekiti wa asasi ya kiraia ya kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Tabora (Tabora Economics and Social Development Organization -TESDO).

Anaitwa Hamisi Masoud Mtwale (sina uhakika na usahihi katika jina la mwisho). Nimeona amejitosa kuomba ridhaa katika Jimbo la Tabora Mjini.

Natamani wenye majina maarufu wakatwe na wapitishwe watu wa hivi. Wengi wamekaa kimaslahi zaidi badala ya kitumishi. Imagine mtu kama Steve Nyerere!!!
IMG-20200716-WA0067.jpg
 
Watu wanachoka ukuu wa mkoa hata Ole Sendeka leo ameamua kwenda kugombe ubunge Simanjiro. Kuna shida kwenye nafasi za wateule wa rais, wanakimbia.
Kwa sababu hawana wito. Walidhani wameenda kuula kama ilivyokuwa zamani. Kwenye hili Jiwe amefanikiwa. Mchwa walijisahau sana!
 
Kwani hauwezi kumfanyia promo mgombea wako bila kujaribu kumshusha au kutumia nyota ya mtu mwingine?
Kibaya zaidi hao watu hawagombei jimbo moja!!

Au nawe unagombea jimboni kwa Mwanry?
Ingekuwa promo ningeenda straight. Nimejaribu kuonesha hali halisi. Wapi nimeongopa? Vijana wa siku hizi bhana.
 
Ingekuwa promo ningeenda straight. Nimejaribu kuonesha hali halisi. Wapi nimeongopa? Vijana wa siku hizi bhana.
Mkuu kuna mahali nimesema unaongopa?

Nilisema unajaribu kumshusha mfano kauli hiyo hapo chini
Umaarufu huo haukuwa na tija bali ulilenga kumjenga mwanasiasa huyu mkongwe kuja kugombea tena ubunge. Siasa za hivi zinaboa!
Sijui ulitumia vigezo gani kusema haukuwa na tija?
Huo unaweza kuwa mtazamo wako tu lakini siyo ukweli au ni ukweli lakini unaohitaji vitu vya kusaidia kuutetea huo msimamo wako kwamba ndiyo ukweli wenyewe. Haitoshi kusema tu hauna au una tija bila maelezo na ushahidi wa ziada.
 
Back
Top Bottom